Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kanisa Katoliki nchini kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), ambapo wamejadili masuala mbalimbali yanayogusa Taifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, Agosti 10, 2026, na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na kusainiwa na Bakari Machumu, mazungumzo hayo yamefanyika katika Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na TEC.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya kitaifa yanayohusu jamii, ikiwemo siasa, imani, maendeleo, pamoja na namna ya kuendelea kujenga na kudumisha amani, mshikamano na ustawi wa Watanzania.
Aidha, Rais Samia amewahimiza viongozi wa Kanisa Katoliki kuendelea kushirikiana na Serikali katika juhudi za kujenga jamii yenye maadili mema, uwajibikaji na mshikamano.
Aidha, Rais Samia amewahimiza viongozi wa Kanisa Katoliki kuendelea kushirikiana na Serikali katika juhudi za kujenga jamii yenye maadili mema, uwajibikaji na mshikamano.
Rais amesema mchango wa viongozi wa dini ni muhimu katika kujenga jamii yenye amani na maadili, pamoja na kuchangia ustawi na maendeleo ya Taifa.






0 Comments