KATIBU WA NEC UCHUMI NA FEDHA AKUTANA NA UONGOZI WA CRDB BANK

 


Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Ndugu Jamal Kassim Ali, leo tarehe 10 Agosti 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa CRDB Bank PLC Dkt. Abdulmajid Nsekela Jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo imelenga kuimarisha ushirikiano kati ya Chama na wadau wake wa kimkakati katika sekta ya fedha, pamoja na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya uchumi, uwekezaji, usimamizi wa fedha na fursa za kukuza shughuli za kiuchumi.

Katika mazungumzo hayo, pande hizo zimejadili pia umuhimu wa kujenga mahusiano endelevu na taasisi za kifedha na wadau wengine wa sekta binafsi katika kuchochea uwekezaji, kuongeza tija na kuimarisha mchango wa shughuli za kiuchumi katika maendeleo.

Ziara hiyo ni sehemu ya hatua za awali za utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Uchumi na Fedha katika kuimarisha ushirikishwaji wa wadau wa kimkakati.

Post a Comment

0 Comments