Mwambande amesema hayo leo tarehe 6 Agosti alipozungumza na Waandishi wa Habari katika banda la DIB kwenye Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela kwenye maonesho ya nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.
Amesema kiwango cha juu cha fidia kinacholupwa ni Mil7.5 kwa mwekaji mmoja endapo Benki itafutiwa leseni na kushindwa kuendelea na shughuli zake.
Amesema " kuna Benki inaitwa Delfis ilifungwa mwaka 2003 nalo zoezi lake la ufilisi liko mwishomwisho" amesema Mwambande.
Aidha amezitaja Benki zingine zilizofilisiwa kuwa kuwa ni FBME Bank, EFATHA,
Convenant For Women (Benki ya Wanawake) hizi zilifungwa 2017 na 18,kuna Benki saba zilifutiwa leseni au zilifungwa ambazo ni Mbinga,Njombe, Meru na Kagera Farmers Corporative Bank.
Amesema zoezi la ufilisi linachukua muda kidogo sababu wengine walikopa ,kuna watu wengine waliweka dhamana mali zao sasa mara nyingi katika kutekeleza hiko zoezi wakati mwingine wengine walienda Mahakamani na lazima haki itendeke kwahiyo unakuta zoezi linachukua muda.
Mwambande ameongeza kwa kusema kuwa kwahiyo ukiangalia kwa Benki za 2017-18 zoezi la ufilisi liko katika hatua tofauti tofauti ziko zingine ambazo zimefanya vizuri sana na zingine zinaendelea taratibutaratibu na mali tulizo kusanya na kuwagawia wale ambao walikua wanadai zaidi ya kiwango ambacho sisi tunatoa.
Mtui amesemakuwa Bodi inaendelea kulipa fidia kwa waliokuwa wateja wa Benki zilizofungwa.
Amesema hivi karibuni Bodi ilitangaza malipo ya mwisho kwa baadhi ya wateja wa FBME Bank, huku amewahimiza ambao hawajachukua fedha zao kufuatilia malipo hayo kupitia ofisi za Bodi zilizopo Benki Kuu (BoT) ya Tanzania Dar es Salaam na Dodoma.
Aidha amesema Benki tisa zimewahi kuwekwa chini ya ufilisi nchini tangu mwaka 2000, huku baadhi ya michakato yake ikiendelea, Bodi ya Bima ya Amana (DIB).
Ameongeza kwa kusema kuwa ufilisi kwa harakaharaka ulitokea baada ya mabenki haya kuwekwa chini ya ufilisi na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ambayo kwa mujibu wa sheria wao ndiyo wanaoweka ufilisi kwa mujibu wa sheria na endapo Benki ikifilisika Bodi ya Bima ya Amana imeichukua.
"Kwa sasa hivi tunaendelea na ufilisi wale wateja ambao hawajachukua amana zao wafike katika Benki ya Biashara wakachukue amana zao kile kiasi wanachofidiwa katika ofisi za matawi ya Tanzania Benki ya Biashara.


0 Comments