Msanii kutoka Zanzibar Bi Fatma Issa aliimba tahadhari na adui kiumbe, daima asikusibu na Mungu akuepushie.
Nyumbu wakiwa wanazaliwa katika eneo la Ndutu huomba sana Mungu awaepushie adui kiumbe kama Fisi, Simba, chui na mbweha ambao nao msimu huo huhamia katika eneo la Ndutu hifadhi ya Ngorongoro ili kuwavizia Nyumbu na watoto wao.
Hata hivyo kwa kuwa Mungu ni wa wote, huwaepusha nyumbu na adui hao kwa kuwa katika safari ya nyumbu, kuanzia wanapozaliwa Ndutu na kuanza mzunguko wa kuhama kila mwaka kuelekea Kenya, hukabiliana na changamoto nyingi za kuliwa na wanyama wala nyama lakini wengi husalimika


.jpg)
0 Comments