MHE.ASHA BARAKA AKUTANA NA MADIWANI KIBAHA 

 

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Pwani kupitia Mashirika yasiyo la Kiserikali (NGO) Asha Baraka amekutana na Madiwani na kuwaahidi ushirikiano katika kufanya kazi bega kwa bega kwa nia ya kukuza jitihada za CCM ndani ya Mkoa na nchi nzima.

Akizungumza na Madiwani wanawake wa Manispaa ya Kibaha  mwishoni mwa wiki kattika mkutano ulioffanyika ofisi za UWT Wilaya  ya Kibaha .

amewapa hamasa ya kukitumikia chama kwa kupitia kutatua na kuzisemea kero za wananchi jambo ambalo litamsaidia Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kusema mambo yote mazuri ambayo yanafanywa katika awamu ya sita.

"Ninyi Madiwani ni wajibu wenu kutatua kero mbalimbali za wananchi katika maeneo yenu pia, tumieni fursa mbalimbali za miradi na uwekezaji ambao unaanzishwa na Mhe.Rais Dkt. Samia" amesisitiza Mhe. Asha Baraka.

Aidha amewasisitiza Madiwani hao kuwa wanaowajibu wa kumsemea na kutangaza miradi mikubwa iliyopo Manispaa ya Kibaha na Mkoa wa Pwani .

Wakizungumza baada ya mkutano huo Diwani wa Viti Maalum Sara Uledi amesema kuwa anatoa shukran kwa Mhe. Mbunge huyo kwa kuwakumbuka na kuahidi watampa ushirikiano wakati wowote ambao watahitajika.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Kibaha Elina Mgonja amesema UWT Wilaya ya Kibaha wamefarijika kwa ujio wa Mhe.Asha na kwamba wanaamini kuwa kuna jambo au mambo mengi mazuri watafanya.

Wakati huohuo naye Diwani wa Viti Maalum Selina Msenga amesema kwa niaba ya Madiwani wenzake wamejifunza na kupata mwanga kuhusiana na masuala ya siasa na kwamba wamechukua uzoefu kutoka kwa mkongwe huyo.

Post a Comment

0 Comments