KAMISHNA BADRU AMETOA PONGEZI  KWA TIMU ZA NGORONGORO ZILIZOSHIRIKI SHIMMUTA


Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bwana Abdul-Razaq Badru amezipongeza timu za Mamlaka hiyo zinazoshiriki mashindano ya Shirikisho la Mashirika ya serikali na Taasisi Binafsi (SHIMMUTA) yanayoendelea mkoani Morogoro kwa kuendelea kulinda na kutangaza taswira ya taasisi hiyo kupitia sekta ya Michezo.


 Akitoa salamu alipotembelea timu hiyo kwa niaba Kamishna Badru, leo tarehe 5 Desemba 2025 Mkoani Morogoro.

Kaimu Meneja wa Uhusiano kwa umma bwana Hamis Dambaya amesema menejimenti ya Ngorongoro imeridhishwa na kazi kubwa iliyofanywa na timu hizo katika mashindano hayo na kulitangaza shirika kupitia utalii wa michezo (sport tourism).

Katika mashindano hayo Ngorongoro imefanikiwa kutwaa Medali saba huku ikidhihirisha upekee wake kimataifa na kuendelea kuwa _Premium Safari Destination._

Post a Comment

0 Comments