Mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi nchini, Luiza Mbutu amefiwa na mumewe, Fari-ala Mbutu ambaye pia ni Mwanamuziki mkongwe amekutwa na umauti jioni ya leo tarehe 25 Desemba 2025 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua na kwa wiki moja.
Luiza ambaye ni Mkurugenzi wa Bendi ya Twanga Pepeta ( CEO) amesema, "Fariala amefariki dunia leo jioni katika Hospitali ya Muhimbili akipatiwa matibabu na kwamba alikuwa anasumbuliwa na presha, lakini ghafla alipata tatizo la tumbo ambalo ndilo limechukua uhai wake."
“Alikuwa anasumbuliwa na presha tu, ila akaja kuumwa tumbo ghafla likavimba, tukampeleka Hospitali ya Muhimbili akafanyiwa vipimo akakutwa na tatizo la mrija wa kupitisha chakula umevimba ikabidi wamfanyie upasuaji wakapunguza utumbo kisha wakaunganisha tena, sasa akawa anaendelea na matibabu ndiyo ameffariki jioni hii,” amesema Luiza.
Luiza na Fariala walifunga ndoa mwanzoni mwa miaka ya 2000 na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Bryan.
Msiba uko nyumbani kwao Salasala jijini Dar es Salaam

0 Comments