WAHITIMU OP MIAKA 6O YA MUUNGANO 832 RUVU WAAHIDI KUWA WAZALENDO

VIJANA wahitimu  wa  mafunzo ya kwa mujibu wa sheria oparesheni  miaka 60 ya Muungano ya kikosi namba 832 KJ Ruvu wameahidi kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kujenga uchumi imara kwa maslahi ya taifa kutokana na mafunzo ya jeshi la awali waliyopata.

Akisoma risala kwa niaba ya Wahitimu wa mafunzo ya Vijana wa Mujibu wa Sheria operasheni miaka 60 ya Muungano 832 KJ Ruvu Hilda Edward amesema kutokana na mafunzo ya wiki 12 waliyopata kujifunza utii, Uzalendo, uadilifu na kuchapa kazi.

wameahidi kuzingatia mafunzo yote kwa kuhakikisha rasimali za nchi yetu hazipotei wakizingatia mafunzo waliyopatiwa katika kipindi chao cha mafunzo.

"Tunaahidi kumuunga mkono Mheshimiwa Rais na Amiri jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan katika kujenga uchumi imara kwa maslahi mapana ya nchi yetu" amesema Hilda.

Amesema yeye na wenzake wanatoa ahadi  kwa Dkt. Samia kwamba watadumisha uzalendo, utii nidhamu  uaminifu  na kwa taifa.

Aidha Wahitimu hao kwa pamoja  wamekula kiapo cha utii kwa Amiri Jeshi Mkuu na kutoa shukrani za  pekee kwa  Wakufunzi wao kwa kuwapatia stadi za maisha katika kipindi chote  cha miezi mitatu walipokuwa Kikosini hapo.

Vijana hao ambao wametoka katika maeneo  mbalimbali wamejifunza  ukakamavu, kilimo na ufugaji, usanii na michezo.

Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Brigedia Jenerali  Solitina  Bernad Nshushi  amesema kuwa  anawapongeza vijana wote kwa kukubali kuja kujifunza mafunzo haya ya kwa mujibu wa sheria kwa sababu kwa kufanya hivyo wamejitende haki  wenye na katika jamii waliyotoka  na taifa kwa ujumla. 

Mwakilishi wa Mkuu wa JKT Kanali George Barongo Kazahura amesema  mafunzo  haya mliyoyapata sasa mmefahamu dhana ya uzalendo mmekua tayari kutumikia taifa popote mtakapokuwa hivyo basi mnapaswa mkatumie elimu hiyo pasipokuvunja utaratibu na  sheria za nchi.

Kamanda  Kikosi cha 832 Ruvu JKT  Kanali  Peter Elius Mnyani amesema vijana waliohitimu  mafunzo yao leo Septemba 4,2024 stadi za maisha elimu hii waliyoipata imewajenga kifikra mbalimbali  za ulinzi na usalama na wamekidhi vigezo.

Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Pwani   Abubakari Kunenge amesema kuwa  vijana wetu  ambao mmehitimu  mafunzo  ya kwa mujibu wa sheria leo nendeni mkatumie fursa mbalimbali  ambazo mmepatiwa.
"Kama jinsi Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan alivyosema katika maadhimisho ya miaka 69 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  kuwa nchi yetu iko salama  vivo hivyo sina budi kusema kuwa kweli hakuna  shaka nchi  yetu  iko salama kiulinzi na usalama  kichumi  pamoja na huduma za kijamii, JKT  ni tanuri linalofunda vijana kuwa wazalendo kwani hata ninapowaangalia  naiona Tanzania  inayoongoza  kiuchumi na vijana wanaotumia
 fursa bila kulalamika hivyo katumieni mbinu za mafunzo mlizopata katika hapa  Kambini   na mkawe mabalozi wema kwa vijana wengine.
Wahitimu hao wakipita kwa ukakamavu.
Kamanda Kikosi 832 KJ Ruvu  Kanali  Peter Elius Mnyani akizungumza kwenye sherehe za kufunga mafunzo ya mujibu wa sheria oparesheni miaka 60 ya Muungano Septemba 4,2024.
Kambi ya 832 KJ Ruvu iliyopo Mlandizi  Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ni kambi teule ambayo imeteuliwa kuchukua makuruta wenye changamoto za kiafya ikiwemo ulemavu wa viungo,ulemavu wa ngozi na wenye changamoto  ya kusikia na kuona.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akizungumza  na wahitimu wa mafunzo ya mujibu wa sheria oparesheni miaka 60 ya Muungano  Septemba 4, 2024 iliyofanyika katika Uwanja wa Mabatini. 
Mwakilishi wa Mkuu wa JKT Kanali George Barongo Kazahura akitoa Salaam zake kwenye sherehe hizo za kufunga mafunzo  kwa mujibu wa sheria oparesheni miaka 60 ya Muungano 832 KJ Ruvu Septemba 4,2024 Mlandizi Mkoani Pwani. 
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi  Brigedia Jenerali Solitina Bernad Nshushi akizungumza  na wahitimu hao huku akiwasisitiza kuzingatia  mafunzo yote waliyopata  kutoka kwa wakufunzi wao pamoja na kulinda afya zao   na afya ya akili.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akikagua gwaride la  wahitimu wa mafunzo ya mujibu wa sheria oparesheni miaka 60 ya Muungano 832 KJ Ruvu Septemba 4,2024 .
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwenye  sherehe za kufunga mafunzo ya mujibu wa sheria oparesheni miaka 60 ya Muungano 832 KJ Ruvu Septemba 4,2024.

Post a Comment

0 Comments