MIl.900 ZATENGWA UJENZI WA MADARASA MANISPAA KIBAHA


 Meya wa Manispaa ya Kibaha Dkt. Mawazo Nicas  akizungumza   katika mkutano na Waandishi wa Habari hawapo pichani leo terehs 10 Desemba 2025.

Na Mwandishi Wetu, Kibaha 

Meya wa Manispaa ya Kibaha Dkt. Mawazo Nicas amesema kuwa uongozi wake pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha wametenga fedha kiasi cha Mil.900 na fedha kiasi cha Mil.400 kwa ajili ya madawati ikiwa ni lengo la kuhakikisha watoto wote ambao wametimiza umri wa kuanza darasa la kwanza wanaanza masomo ifikapo mwakani.

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano katika Manispaa ya Kibaha Dkt Nicas amesisitiza kwa kusema kuwa kiasi cha Mil. 900 ambacho nikwa ajili ya ujenzi wa madarasa huku Mil. 400 kimetengwa kwa ajili ya kutengeneza madawati ya wanafunzi watakao anza masomo ifikapo mwakani 2026.

"Mil.400 tayari zimeshatoka na baada ya kukamilika tutawaitamje kushuhudia kwenyen mgawanyo wa shule. 

"Tutasimamia katika kuhakikisha aliyechukua tenda ya kutengeneza madawati hayo anatengeneza kwa kuzingatia ubora na thamani na fedha aliyolipwa" amesema Meya Dkt. Nicas.

 " Tutasimamia wenyewe na mimi nikiwa Kiongozi naahidi kuwa sitatoa wala pokea rushwa na Mhe.Rais anasisitiza hili jambo litekelezwe kwa vitendo hivyo basi natoa angalizo endapo watatengeneza madawati hayo chini ya kiwango watachukuliwa hatua kali" amesema Meya wa Kibaha Dkt. Nicas.

Aidha Meya Kibaha Dkt. Nicas amesema kuwa kila kata imepewa kiasi cha Mil.30 kwa ajili ya kuchonga barabara za mitaani huku amewatoa hofu wananchi kwamba ambao bado hawajaona maendeleo katika mitaa yao wasiwe na hofu kwani fedha bado zipo na wanakwenda kuangalia namna ya kuratibu matumizi yake ili wananchi waweze kupata huduma ya kuchongewa barabara katika mitaa yao ili ziweze kupitika katikakipindi cha mwaka mzima.

Wakati huohuo Meya wa Manispaa ya Kibaha Dkt. Nicas amewapongeza wananchi wa Kibaha kwa namna walivyoonesha utulivu katikakusherehekea kumbukumbu ya miaka 64 ya Uhuru wa Tanzania.

" Kwa sasa tunakwenda na slogan ya siku 100 za Mhe. Rais Dkt .Samia ambapo tumeelekezwa watoto waliofikia umri wa kwenda Shule waende hivyo tumejipanga vizuri wote waliofaulu darasa la saba hasa Manispaa ya Kibaha wamefauli kwa kiwango cha asilimia 100 wote watakwenda Shule Sekondari hakuna atakayeachwa.

"Katika Manispaa ya Kibaha awali waliofaulu walikua wanafunzi 

3 ,000 sasa idadi imeongezeka na kuwa 6,000 ndiyo sababu tumelazimika kuongeza madarasa na madawati,fedha ipo ya kutosha tunaishukuru serikali yetu kuwa hakuna mtoto atakaye kosa nafasi wala kuachwa" amesema Meya Dkt. Nicas.

" Tunatarajia ndani ya siku 60 ujenzi wa madarasa utakamilika,na inasisisitiza kwa kusema kuwa Mhe.Rais Dkt Samia anastahili pongezi nyingi kutokana na kufanya maajabu katika kipindi.cha uongozi wake kwa kuleta maendeleo mengi na yaanyoonekana nchini .

Post a Comment

0 Comments