SHEIKH JUMUIA YA SHIA TANZANIA ATOA SALAMU ZA KRISMAS I

Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania TIC Maulana Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge Ametoa salamu za Krismas kwa Wakristo.

Sheikh Jalala Amesema " Krismas ya mwaka huu iwe ni sababu ya kuwaasa vijana kutambua umuhimu wa nchini yao na kuwa wazalendo kwa nchi yao na iwe sababu ya Watanzania kuvumuliana na kuishi kwa Amani na Upendo."

Sambamba na hilo Mshauri wa Sheikh Mkuu Mzee Azim Dewj amesema  Krismas ya mwaka huu itumike kutoa mafunzo kwa vijana maana miongoni mwa kazi za Taasisi za dini ni kutoa mafunzo ya maadili mema kwa wananchi kwa ujumla. 

Post a Comment

0 Comments