Na Mwandishi Wetu, Rombo.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeshiriki katika tamasha la Rombo Marathon_ lililofanyika leo tarehe 23 Desemba 2025, Rombo Mkoani Kilimanjaro na kuvutia wageni kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Ushiriki wa Ngorongoro Rombo Marathon ambayo pia watumishi wa Mamlaka hiyo wameshiriki mbio za umbali tofauti inadhihirisha jitihada za mamlaka hiyo kuunga mkono sekta ya michezo, kutangaza vivutio vya utalii kupitia utalii wa michezo, kujenga uhusiano na wadau kupitia matukio ya kijamii na kitaifa na kimataifa.
Sambamba na kushiriki katika tamasha hilo, wananchi waliohudhuria mashindano hayo walipata fursa ya kutembelea banda la Ngorongoro lililowekwa mahsusi kwa ajili ya kutoa elimu kwa washiriki na wananchi kwa ujumla kuhusu shughuli za Uhifadhi na utalii pamoja na mchango wa hifadhi ya Ngorongoro katika kulinda urithi wa asili na wa kitamaduni.


0 Comments