Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Rais Wastaafu wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Ali Shein wa Awamu ya Saba na Amani Abeid Karume wa Awamu ya Sita, Ikulu Zanzibar.
Marais hao wastaafu wamemtembelea Rais Dkt. Mwinyi kwa lengo la kumpongeza kwa ushindi wa kishindo alioupata, pamoja na kupongeza hali ya amani na utulivu iliyoshuhudiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu.

0 Comments