Hospitali ya Taifa Muhimbili -Mloganzila imeendelea kuboresha huduma katika wodi za watoto wachanga kwa kuongeza vifaa tiba na kuimarisha uwezo wa watoa huduma ili kuhakikisha watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wana nafasi kubwa ya kuishi na kukua vizuri.
Kauli hiyo imetolewa na Dkt. Lucy Mpayo, Bingwa Mbobezi wa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati , alipokuwa akizungumza katika matembezi ya kuadhimisha Siku ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati Duniani yaliyofanyika hospitalini hapo yenye kauli mbiu;“Tuwapatie mwanzo bora watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya wakati kwa afya bora”.
Ameeleza kuwa maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka Novemba 17, kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu changamoto wanazokutana nazo watoto hao na kuhamasisha hatua za kuboresha huduma zao.
https://www.instagram.com/p/DRJytUyDHC3/?img_index=9&igsh=ZXp3Mmp1OXYwZGxr

0 Comments