BAKWATA:SWALA YA EID EL FITR KITAIFA ITASALIWA DAR


 Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limewajulisha Waislamu na wananchi wote kwa ujumla kuwa Sikukuu ya Eid El-Fitri itakuwa Machi 20 au 21, 2026 itategemeana na mwandamo wa mwezi.

Vile vile BAKATWA wameeleza kuwa sherehe za  Eid El-Fitri kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika Mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa upande mwingine taarifa ya BAKWATA  iliyotolewa leo tarehe 12  Machi 2026 ambapo  imeeleza  kuwa Swala ya Eid  El Fitr itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI BAKWATA Makao Makuu Kinondoni kuanzia saa 1.30 asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre Posta Jijini Dar es Salaam , kuanzia saa 09.00 mchana Inshallah.

Post a Comment

0 Comments