MUHIMBILI MLOGANZILA YATOA MAFUNZO YA KUHUDUMIA WANAOHITAJI UANGALIZI MAALUM KWA WAFIZIOTHERAPIA KUTOKA BABATI NA SONGEA

Wahitimu wa mafunzo maalum ya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila wametakiwa kutumia ujuzi na maarifa waliyopata kuwahudumia wananchi ili kuendelea kuboresha huduma za afya zinazopatikana katika maeneo yao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Tiba MNH-Mloganzila, Dkt. Elineema Meda wakati akihitimisha mafunzo ya mwezi mmoja yaliyoratibiwa na Kitengo cha Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu hospitalini hapo.

“Serikali imefanya jitihada za kutosha za kuboresha huduma za afya nchini, hivyo ni wajibu wa watoa huduma kuwa wabunifu na kubadilishana uzoefu, unapopata mafunzo wewe ukirudi washirikishe wenzio katika eneo lako la kutolea huduma ili wote kwa pamoja muweze kutoa huduma bora kwa Watanzania wenzetu bila kujali mahali walipo” amebainisha Dkt. Meda

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Utafiti, Mafunzo na Ushauri wa Kitaalamu, Dkt. Mwanaidi Amiri amesema hospitali itaendelea kushirikiana na wataalam wake pamoja na wadau wengine kuanzisha mafunzo mbalimbali kwa lengo la kuendelea kuboresha huduma kwa Watanzania.

Naye Mkuu wa Idara ya Fiziotherapia na Utengemao PT Patrick Foster amesema mafunzo hayo yamejumuisha nadharia na vitendo na wahitimu walifanya majaribio mbalimbali na kufaulu, watakuwa mabalozi muhimu kwa kuwa utendaji wao utabadilika.

Aidha, PT. Renalda Massawe, mhitimu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea ameupongeza uongozi wa Hospitali ya MNH Mloganzila kwa kubuni na kutoa mafunzo hayo kwakuwa yana manufaa makubwa kwa watoa huduma hususan katika kipindi hiki ambacho kuna mabadiliko ya utaoji wa huduma

Post a Comment

0 Comments