MAIKO SALALI WA FDH AINGIA KINYANG'ANYILO CHA UBUNGE JIMBO LA MPWAPWA


Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Foundation for Disability Hope FDH Maiko Salali, ameingia rasmi kwenye kinyang’anyiro cha

kugombea Ubunge kwa

 kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Jimbo la Mpwapwa katika uchaguzi ujao.

Salali amechukua fomu hiyo leo katika ofisi ya CCM Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma  leo tarehe 30 Juni 2025 mbele ya viongozi wa chama, wanachama na wafuasi wake waliokusanyika kushuhudia tukio hilo.

Salali anajiunga na orodha ya wanachama wa CCM wanaowania ridhaa ya kugombea ubunge kupitia chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu, huku Jimbo la Mpwapwa likitarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na mvuto wake wa kisiasa.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo Tinge amesema nauli mbiu yake ni Ububunifu,ushawishi,ushirikishaji na uthububutu kuziendea changamoto na kuwa fursa.

 

Post a Comment

0 Comments