THRDC WATOA MAJAKETI YA UTAMBULISHO KWA WAANDISHI WA HABARI WA MISA TZ

MISA Tanzania imepokea Press Jackets toka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) Kwa ajili ya usalama wa waandishi wa habari kuelekea uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Mratibu wa THRDC Onesmo Olengurumwa- amekabidhi press Jackets hizo Kwa Mwenyekiti wa MISA Tanzania  Edwin Soko wakati wa mafunzo yakuwajengea uwezo Waandishi wa Habari kwenye kujua sheria za uchaguzi kwenye hotel ya ukumbi wa Mbezi Garden Jijini Dar es salaam 

Mwenyekiti Edwin Soko ameishukuru THRDC na kusisitiza kuwa  ushirkiano baina ya taasisi hizo mbili utaendelea kuwepo kwa lengo la kulinda uhuru wa habari na usalama wa waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Post a Comment

0 Comments