KABUDI ANADI FURSA TASNIA YA FILAMU INDIA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amenadi fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo hapa nchini  kwenye Sekta ya Sanaa hususani tasnia ya Filamu.

Mhe. Kabudi ametangaza fursa hizo wakati akihutubia mkutano wa Majadiliano na Vyombo vya Habari vya Kimataifa ( Global Media Dialogue) uliofanyika jijini Mumbai leo Mei 2, 2025.

“ Kwa miaka mingi Tanzania imekuwa kitovu cha maeneo yenye mvuto kwa ajili ya kupiga picha na kuandaa filamu kama vile Mlima Kilimanjaro, Mbuga za wanyama za Serengeti, Ngorongoro  na kisiwa cha Zanzibar, hivyo tunawakaribisha wawekezaji kutoka India hususani kutoka Bollywood kutumia vivutio hivi kuandaa filamu” Alisisitiza Mhe. Kabudi.

 Mhe. Kabudi pia alitoa wito kwa wadau wa sekta za Sanaa na Habari kuwekeza nchini Tanzania kutokana na uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji na soko la uhakika linalochagizwa na idadi kubwa ya watu.

Mkutano wa Global Media Dialogue umefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Kimataifa wa Wadau wa Ubunifu, Habari na Burudani wa ‘’World Audio Visual and Entertainment Summit (WAVES)’’ unaofanyika jijini Mumbai, India kuanzia tarehe 1 - 4 Mei, 2025.

Mkutano huo unaohudhuriwa na mawaziri na wadau wa Sekta za Ubunifu, Habari na Burudani kutoka mataifa mbalimbali dunia unalenga kujuadili mchango wa Sekta za Habari, Ubunifu na Burudani katika kukuza uchumi umezinduliwa tarehe 1 Mei, 2025 na Waziri Mkuu wa Serikali ya India Mhe. Shri Narendra Modi.

Mhe. Mchengerwa aweka jiwe la msingi jengo la jiji Arusha, ashuhudia utiaji saini mikataba ya miradi ya bilioni 40

Post a Comment

0 Comments