MEJA JENERALI MABELE AMEWEKA JIWE LA MSINGI NYUMBA ZA KULALA WAGENI BUSTANI YA WANYAMA RUVU JKT


Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa  (JKT) Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele kushoto na Mkuu wa Kikosi Cha 832KJ Ruvu  Kanali Peter Elius Mnyani. 

Kabla ya kuweka jiwe  jiwe la msingi katika nyumba hizo , alikuwa mgeni rasmi katika  sherehe za kufunga  mafunzo ya  ya JKT  kwa vijana wa kujitolea Operesheni Miaka 60 ya Muungano 832KJ Ruvu iliyofanyika   Aprili 17 2025 kwenye viwanya vya Ruvu Rest House .
Mkuu wa Jeshi  la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele akimlisha Ndege Mbuni anayefugwa kwenye bustani  ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.   
Meja Jenerali  Rajabu Nduku Mabele ameweka jiwe la msingi kwenye nyumba nane   za kulala watalii zenye uwezo wa kuchukua watu wawili kila nyumba moja. 

Nyumba hizo zinanajengwa mahsusi kwa ajili ya wageni wataokwenda kutembelea katika bustani ya wanyama ya Ruvu JKT, iliyopo Mlandizi  Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

Mkuu huyo wa JKT   akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya  kuweka jiwe la msingi amesema kuwa ujenzi huo ni katika kuipandisha thamani  bustani hiyo ya wanyama  kwa sababu kwa sasa inatembelewa na watalii wengi pia   imekua kivutio kikubwa kwa wakazi wa Mikoa jirani  na Mkoa wa Pwani ambao hufika kuona wanyama wapole walioko kwenye bustani hiyo.

"Mradi wa Bustani kama huu umezinduliwa Mbweni JKT, ikiwa ni  katika kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutangaza utalii kwa kupitia filamu yake ya Royal Tour na matunda yake yanaonekana watalii wameongezeka  nchini.

"Kwa kupitia mradi huu Kikosi tunapata kipato kutoka kwa   watu mbalimbali wanaokuja kuwaona wanyama  na tutaongeza wanyama rafiki na siyo wanyama  wakali" amesema Meja Jenerali Mabele.

Akizungumzia kuhusu kuongeza bustani za wanyama amesema kuwa endapo  kuna Kikosi kingine kutakuwa na  mazingira rafiki  ya kuweka bustani ya wanyama watafanya hivyo sababu hii ninfursa adhimu.

"Tunawakaribisha wageni wote wa ndani na nje ya nje waje kuona wanyama  wetu  kabla ya kwenda kwenye mbuga kubwa kuona wanyama wengine" amesema Meja Jenerali Mabelle.

Wakati huohuo vijana waliohitimu mafunzo ya Oparesheni  Miaka 60 ya Muungano ambao walipita mbele ya mgeni rasmi na gwaride kwa mwendo pole na wa haraka ,kwata singe,kufungua silaha na kufunga aina ya SMG,Kwata za miguu,Kwaya,Ngoma na 'Live Band'.

Meja Jenerali Mabele aliyekua mgeni  rasmi ametoa zawadi kwa  wahitimu waliofanya vizuri katika mafunzo ambao ni  Kuruti aliyefanya vizuri  katika nyanja zote  Mussa Mussa mwingine aliyepata zawadi ni Kuruti  Juma Chacha  Wambura ameshinda medani ya shabaha huku na  Suma Mwakatundu ambaye amepata zawadi ya medani ya  porini.

Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu  wengine Lucia Mushi  amesema kuwa wanaahidi  watatumia mafunzo hayo kwa maslahi ya taifa na  endapo watahitajika itakuwa ni fursa kwao huku wakisisitiza watakilinda kiapo chao.

Akizungumza na wahitimu wa mafunzo  hayo Kamanda wa Kikosi 832 KJ Ruvu Kanali Peter Elius  Mnyani amewaasa vijana kukilinda kiapo chao walichoapa sambamba na kutunza afya zao kwa sababu ndiyo mtaji wao wa kesho.

Kanali Mnyani amesema kuwa vijana hao walianza mafunzo yao  tarehe Desemba 30, 2024.

"Nawaasa vijana kutunza afya zenu kwani mtaji wa masikini ni nguvu zake lakini ninyi nguvu mnazo"amesema Kanali Mnyani.

"lindeni afya zenu  na afya ya akili hapo mtaweza kulinda taifa lako kikamilifu" amesema Kanali Mnyani.

Aidha sherehe hizo zimehudhuriwa na Mwakilishi wa CDF Brigedia Jenerali Abubakari Chalo, Kanali Makame Daima wa Jeshi la Kujenga Uchumi  Zanzibar (JKU), Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kibaha Mkoa  wa Pwani. 

Post a Comment

0 Comments