Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amekemea na kulaani udhalilishaji uliofanywa na mabinti kadhaa walioshirikiana kumdhalilisha binti mwenzao.
Katika taarifa yake Waziri Gwajima amelaani tukio hilo na kusema hatua Kali dhidi ya wasichana hao waliomdhalilisha mwenzao zinachuliwa..
Taarifa iliyotolewa na Waziri Gwajima leo April 20,2025 inasomeka hivi:,
Usiku wa kuamkia leo zimevuja video za wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini wanaosadikika kugombania mwanaume ambapo kwenye video hizo mwanaume huyo anayegombaniwa ametajwa kwa jina la mwijaku. Kupitia ukurasa wa instagram wa mwanadada mange kimambi ambapo video hizo zimepostiwa inasadikia wanafunzi hao ni kutoka chuo kikuu cha udsm na ardhi (Mpigaji ni mwanafunzi wa UDSM anayefahamika kwa jina la MERRY GERVAIS @marrriie_y_ , anaepigwa ni mwanafunzi wa Ardhi. It seems wanashare hostel moja, then Mwijaku kaenda kawalala wote wawili. Alafu it seems Mwijaku ndo kamchoma kwa wenzie).
Baada ya video hizo kusambaa kwa kasi waziri mwenye dhamana ya maendeleo ya jamii, jinsia , wanawake na watu wa makundi maalumu DOROTH GWAJIMA kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika-;
"Pamoja na Heri ya Pasaka kwenu wote, nasikitika kuwapa taarifa kuwa, usiku wa kuamkia Jumapili ya Pasaka tarehe 20.4. 2025 nilipokea tags nyingi kupitia mtandao wa Instagram wakinitumia video kadhaa zinazoonesha mabinti kadhaa wakishirikiana kumdhalilisha binti mwingine kwa maneno na vipigo na mambo mengine mabaya ambapo, watoa taarifa walidai kuwa, mabinti hao wote ni wanafunzi wa vyuo vikuu viwili tofauti nchini huku wengine wakidaiwa kuwa, wanasoma darasa moja na huyo binti wanayemdhalilisha na kumrekodi. Aidha, kwenye mazungumzo yao kama yanavyosikika, inaonekana ni ugomvi wa kumgombania mwanaume anayetajwa kwa jina moja la Mwijaku.
Binafsi, nimesikitishwa sana kusikia mabinti wasomi ambao, wangetakiwa kujikita kwenye elimu na kuunganisha nguvu kupambana kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto badala yake wanatumia nguvu zao na elimu zao kukatiliana, kudhalilishana na kujidhalilisha wao kwa wao. Udhalilishaji waliofanya kwa Binti mwenzao haukubaliki kabisa na unastahili kukemewa kwa nguvu zote, kwani ni kinyume na sheria zote na pia siyo utu wala siyo haiba ya mwanamke wa Dunia ya sasa kwamba, akipishana jambo na mwanamke mwenzie au mtu yeyote, basi amfanyie udhalilishaji kwani, huko ni kujidhalilisha yeye mwenyewe na kudhalilisha wanawake wote.
HATUA:
1. Nimewasiliana na manusura na kumuunganisha na huduma za ustawi wa jamii, msaada wa kisaikolojia na huduma za Dawati la Jinsia Polisi ambapo, pia atapata Msaada wa kisheria ili haki itendeke.
2. Nawasiliana na Wakuu wa Vyuo husika kupitia Madawati ya Jinsia kwenye Vyuo husika Ili hatua za nidhamu zichukuliwe.
3. Nawasiliana na Waziri mwenye Dhamana na Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani kwa hatua zaidi.
WITO: tuache kumaliza migogoro kupitia utaratibu wa kudhalilisha wengine. Aidha, wanawake wenzangu wote, hima tulinde heshima na haiba yetu kwa kuungana kutokomeza ukatili wa kijinsia na kwa watoto huku sisi wenyewe tukijitenga na hatua za kukatili na kudhalilisha wengine. HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA."
NB: UKATILI WA KIJINSIA HAUKUBALIKI KWA NAMNA YOYOTE ILE HAIJALISHI NI JINSIA GANI


0 Comments