Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mara, kwenye kikao cha ndani kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Mara, leo Jumatano tarehe 23 Aprili 2025, akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku tano, mkoani humo.
Ziara ya Balozi Nchimbi mkoani Mara inahusisha pia kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025, kupitia miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo, zinazotekelezwa na Serikali ya CCM, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano na Mwenyekiti wa CCM, katika kuwatumikia wananchi.





0 Comments