SERIKALI YA TANZANIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA USAFIRISHAJI

 Msemaji Mkuu wa Serikali alifanya ziara muhimu katika eneo la bandari kavu ya Kwala, mradi mkubwa wa kimkakati unaolenga kuimarisha usafirishaji na biashara nchini Tanzania. 

"Ziara hii ilikuwa na lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi na kutoa taarifa kwa umma kuhusu hatua zilizofikiwa na faida za mradi huu muhimu."

"Akizungumza na 

Waandishi wa Habari, Msemaji Mkuu wa Serikali alieleza kuwa bandari kavu ya Kwala ni mradi muhimu katika kupunguza msongamano katika bandari ya Dar es Salaam na kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo. Amesisitiza kuwa mradi huu utachochea ukuaji wa uchumi wa viwanda na kuongeza ajira kwa Watanzania.

"Ameongeza kwa kusema kuwa serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya usafirishaji ili kuwezesha biashara na kuchochea maendeleo ya kiuchumi. 

Aidha ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano katika miradi ya maendeleo ya nchi, akisisitiza kuwa mafanikio ya miradi hii ni mafanikio ya Watanzania wote."

Post a Comment

0 Comments