PATCHO MWAMBA KUTOA DOCUMENTARY 2025

Imeandaliwa na FM Academia


 Walden 'Black Mamba'

Hilo si jina geni kwa wafuatiliaji wa mambo, alikua ni mmoja ya askari (mwanajeshi) shupavu na mstari mbele ktk vita, Kubwa zaidi huyu alikaa kwenye maji siku kadhaa (Mto Kagera) akifanya yake.


Yapo mengi ya kumwelezea huyo na wengine wengi, lakini sisi *FM Academia* tunae *Patcho Mwamba.*


*Patcho Mwamba* wote tunamfamu wakubwa kwa watoto vijana kwa Wazee Makundi yote kutokana na umahiri wake ktk mziki na Uigizaji.

*Patcho Mwamba* ni Kiongozi c mtawala, greda mfungua njia na kusimamia, sifa Kuu ya Kiongozi uwe na ngozi ngumu na masikio Makubwa vyote *Patcho* anavyo pamoja na mishale mingi lakini anasimama imara kama Kiongozi na anasikiliza.

"Naweza kuelezea mengi juu ya *Patcho Mwamba* tokea anafika anaanza na bendi ipi aliishi  wapi kwa nani nyumba gani, mchumba wa kwanza kwa nchini Tanzania".

Ndiyo maana *Patcho Mwamba* mwenyewe kakubali kutengeneza *Documentary* yake ambayo mwaka huu mambo yakienda vizuri itakamilika na itasambazwa bure kabisa kama zawadi na kujifunza pia aliyopitia kwa hapa Tanzania hadi sasa.

Leo ni *Siku yake ya Kuzaliwa Patcho Mwamba Tajiri,* niwaombe Sana Ndugu zangu tumtakie heri ktk siku yake hii muhimu Mwenyezi Mungu azidi kumbariki ampe Afya njema na baraka tele.


Post a Comment

0 Comments