Mkutano huo umefanyika katika eneo la Vigwaza Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ambapo Waandishi wa Habari wameona utekelezaji wa Serikali ikiwa ni pamoja na kumetembelea eneo la hifadhi ya viwanda la Sino -Tan ambalo lengo ni kuwaonesha Watanzania kupitia vyombo vya habari, maendeleo ya makubwa ya mradi huu na utekelezaji wa miradi mingine ya Serikali ndani ya kipindi cha miaka minne (4) ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Kipekee naomba nitumie fursa hii kuwashukuru sana ninyi Wanahabari wenzangu na vyombo vyote vya habari nchini kwa kuendelea kujitokeza kwa wingi katika mikutano ya Msemaji Mkuu wa Serikali inayoendelea Jijini Dodoma na mikutano hii ambayo tumeamua kuihamishia uwandani kwenye maeneo inakotekelezwa miradi" amesema Msigwa.
"Natumia nafasi hii kipekee kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake na kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea maendeleo Watanzania; Sote ni mashuhuda wa miradi mikubwa iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa kwa lengo la kuboresha huduma na kuwaletea maendeleo Watanzania" amesema.
Msigwa amesema ndugu wanahabari, naomba nitumie fursa hii pia kuwashukuru viongozi wa Wizara ya Uchukuzi (Wakiongozwa na Mheshimiwa Waziri Prof. Makame Mbarawa Mnyaa), Kituo cha Uwekezaji Tanzania – TIC (Wakiongozwa na Mtendaji Mkuu Gilead Teri) na Mkoa wa Pwani (Wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Bw. Aboubakar Kunenge) kwa kutupa fursa ya kufanyia mkutano wetu katika eneo hili la mradi".
Aidha, nawapongeza Wahandisi na watalaam wote wanaosimamia utekelezaji wa mradi huu kwa niaba ya Watanzania amesema Msigwa.
Baada ya utangulizi huu naomba nieleze kuwa mkutano wetu wa leo utajikita katika kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo yaliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya sita.
Shughuli za uwekezaji katika sekta ya viwanda na mafanikio yaliyopatikana kutokana na uwekezaji huo katika kipindi cha miaka minne.
Maendeleo ya ujenzi wa eneo la Bandari Kavu ya Kwala, kongani ya viwanda, Bandari Kavu (ICDs) na maendeleo mengine,
Pia amezungumzia kuhusu mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe na sura ya Kitaifa ya utekelezaji wa miradi mingine mikubwa ya maji nchini,
5. Maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Dar - Chalinze – Morogoro,
6. Utekelezaji wa Bajeti ya Mkoa wa Pwani kwa mwaka 2024/25 na matarajio ya bajeti ya mwaka 2025/26, na miradi mikubwa iliyotekelezwa mwaka 2024/25 thamani yake na ufanisi wake.
Wakati huohuo Msemaji Mkuu wa Serikai amezingumzia utaratibu utoaji wa vitambulisho vya kidigitali kwa Waandishi wa Habari (Digital Press Cards).
0 Comments