Kibaha Pwani
Kiwanda Cha Doweicare kilichopo eneo la Lulanzi Picha
yandege Wilayani Kibaha wametoa mchango wa fedha ikiwa katika kuchangia ujenzi wa kalavati.
Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bob Chen amesema kuwa wamekabidhi kiasi cha Sh.500,000 kwa Uongozi wa Serikali ya Mtaa ya Lulanzi huku akisisitiza kw akusema kuwa wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii Wilayani hapa na ndani ya Mkoa wa Pwani kwa ujumla.
Doweicare ambao ni wazalishaji wa taulo za kike (Softcare Sanitary Pads) tunayofuraha kubwa kurejesha kwa jamii japo itaonekana ni kidogo lakini tunayorekodi ya kuchangia huduma nyingi " amesema Chen.
Chen amesema kuwa wanapokuwa na nguvu wanachangia na hata pindi daraja litakapokamilika watakuwa sambamba.
"Natoa wito kwa wwawekezaji wengine wote ndani ya Wilaya ya Kibaha na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kwamba wanao wajibu wa kutoa msaada katika maeneo ya jirani na jamii zinazowazunguka" amesema Chen.
Asilimia 57.5 ya gharama ya mradi huo imetolewa na kiwanda cha Doweicare.
Akizungumza leo tarehe 5 Februari 2025 Mwenyekiti wa Mtaa wa Lulanzi Thobias Shilole amewaeleza Waandishi wa Habari kuwa wanashukuru kwa mchango huo kwani eneo hilo limekuwa korofi kupitika hasa nyakati za mvua.






0 Comments