Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kuwa maandalizi ya kufanya biashara saa 24 sokoni Kariakoo yako ukingoni na uzinduzi utafanyika tarehe 22 Februari 2025.
"Hivi sasa tuko katika hatua za kufunga taa na camera za usalama ikiwa ni kwa ajili ya kuimarisha usalama wa watu na mali zao" amesema Chalamila.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Januari 30,2025 katika ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana RC Chalamila amesema Jiji hilo ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi hivyo Februari 22 mwaka Mkoa huo utazindua rasmi mpango wa shughuli za kibiashara kufanyika saa 24.
Akizungumzia Mkutano wa Nishati wa wakuu wa Nchi za Afrika RC Chalamila amewashukuru na kuwapongeza wananchi wa Mkoa huo kwa ushirikiano mkubwa walioutoa ikiwemo kuimarisha amani, utulivu na usafi hivvyo ameelekeza Wilaya zote kuendelea kusimamia suala la usafi ili Mkoa uendelee kuwa kivutio huku akisisitiza kuwa Serikali inakusudia kuanza kutumia usafiri wa treni na majini kuimarisha usafiri ndani ya Jiji hilo.
Mwenyekiti wa bodi ya soko la kariakoo Hawa Ghasia amesema kuanzia januari 31 wanaanza kuweka majina ya wafanyabiaahara ambao walikuwepo kwenye soko la kariakoo kabla halijaungua ili wasajiliwe na kwamba baada ya hapo watasajili wafanyabiashara wapya na waliokuwa wanadaiwa wanapaswa kulipa madeni yao.
0 Comments