PWANI WAITWA KUBORESHA TAARIFA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Chifu wa Mkoa  wa Pwani Salim  Mashiba akiwa kwenye  picha ya pamoja na Meza kuu leo tarehe 01 Februari 2025 baada ya kupata mafunzo ya siku moja kutoka Tume  ya Uchaguzi. 
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa  ya Uchaguzi  Mhe.Jaji (Rufaa) Mbarouk  S. Mbarouk amesema wananchi wanatakiwa kujitokeza  kuboresha taarifa zao  kwenye daftari la mpigakura  ndani ya siku saba ambapo ni kuanzia Februari 13 hadi 19 2025 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia  saa mbili asubuhi  na kufungwa saa 12 jioni. 

Mhe.Jaji Mbarouk amesema  hayo leo tarehe 1 Februari  2025  kwenye mkutano  na wadau  wa uchaguzi  kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwenye mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

"Tume katika kuhakikisha inakwenda sambamba na  na mabadiliko ya teknolojia  ikiwa ninpamoja na  kurahisisha  zoezi  hili  uboreshaji wa daftari,imeboresha mfumo wa uandikishaji ambao mara ya kwanza  utamuwezesha mpiga kura aliyepo kwenye daftari  kuanzisha  mchakato wa kuboresha taarifa zake au kuhama kituo kwa kutumia aina yeyote  yq simu ya kiganjani au kompyuta" amesema Mbarouk.

Amesema kuwa anawakumbusha wadau na wananchi  kwamba  kujiandikisha kuwa mpiga kura  zaidi ya mara moja  ni kosa  la jinai kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 114(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani Na.1 ya mwaka 2024.
Amesema kifungu  hicho kinaeleza  kuwa mtu yeyote atakayeomba kuandikishwa zaidi ya mara moja atakuwa ametenda kosa  la jinai  nanakitiwa hatiani  adhabu  yake  ni faini isiyopungua  miezi  sita  jela na kisichozidi  miaka miwili gerezani au vyote kwa pamoja  yaani kulipa  faini na kifungo gerezani.

Amesema kuwa wadau mliopo haoa nendeni mkawaelimishe wananchi  kwamba  wakajiandikishe mara moja kwenye  Kituo kimoja  ili kuepuka uvunjaji wa sheria.

"Kwa kuzingatia  masharti  ya kifungu ya kifungu cha 168 cha Sheria ya Uchaguzi  wa Rais ,Wabunge na Madiwani Na.1 ya mwaka  2024 kadi za mpiga kura  zilizotolewa mwaka 2015 na 2020 zenye  jina  la Tume  ya Taia ya Uchaguzi  ni halali na zitaendelea kutumika  kwenye chaguzi zijazo.

"Zoezi hili la  uboresha wa Daftari  haliwahusu wapiga kura  wenye  kadi hizo na  ambao kadi zao  hazijaharibika au kupotea au hawajahama  kutoka  eneo moja  la uchaguzi kwenda  eneo  jingine au taarifa zao hazijakosewa au hawahitaji kuboresha taarifa zao.
Amesema kuwa Tume imeweka utaratibu  kwa watu wenye  ulemavu ,wazee, wagonjwa,wajawazito na wakina  mama wenye  watoto wachanga  watakaokwenda nao vituoni kupewa fursa ya kuhudumiwa  bila kupanga foleni,tunawaomba  wadau wa uchaguzi  muwafahamishe  wananchi  wote waliopo kwenye makundi tajwa kujitokeza kwa wingi  kwenda  kujiandikisha  au kuboresha taarifa zao vituoni kwa kuwa  kumewekwa utaratibu mzuri wa kuwahudumia" amesema Mhe. Mbarouk.

Amesema  kuwa kila Chama Cha Siasa  kimepewa   nakala ya orodha vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura huku dhumuni la kuwapatia nakala hizo ni kuwawezesha kupanga  na kuweka  mawakala  wa uandikishaji katika vituo vya  kuandikisha  wapiga kura.
Imeelezwa kuwa kila Chama  Cha Siasa  kitaruhusiwa kisheria  kuweka  wakala mmoja  kwenye Kituo  cha kuandikisha  wapiga kura  kwa lengo  la  kushuhudia  utekelezaji  wa  zoezi  la uboreshaji  kituoni ikiwemo kuwatambua  wale wanaokuja Kituoni  kama wana sifa za kuandikishwa.

"Mawakala  au Viongozi  wa Vyama  vya Siasa  hawaruhusiwi kuingilia  mchakato  wa  uboreshaji wa Daftari  la Kudumu la Mpigakura Kituo ni hivyo nawaomba  Viongozi  wa Vyama Siasa na wadau  wa uchaguzi  kwa  ujumla  kuzingatia Sheria  ya Uchaguzi, Kanuni, za Uboreshaji  na maelekezo ya Tume na kusimamia miiko na mipaka  ya uendeshaji wa zoezi  la uboreshaji wa Daftari. 

Kauli mbiu ya uboreshaji  wa Daftari  la Kudumu la Wapiga Kura kwa mwaka 2024/25 inasema Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi  wa Uchaguzi. 

Post a Comment

0 Comments