TAKUKURU YAWABANA WAKWEPA USHURU KIBITI


Kibaha,Pwani
Taasisi  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani imefanikisha kuongeza makusanyo Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani  kwa kipindi cha Oktoba  hadi Desemba 2024.

"Tulifanya  uzuiaji  katika  mfumo wa kukusanyaji  wa mapato kwa kutumia POS mashine  kwa kuongeza makusanyo  kutoka 4,632,682.75 kwa wiki  hadi Sh.Mil.12,089,760 ambapo kwa mwaka  makusanyo yatakuwa MI.480,000,000.
Hayo yamesemwa leo tarehe 31 Januari  2025 na  Kamanda wa TAKUKURU  Mkoa wa Pwani Alli Sadiki (Pichani juu) alipozungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika ofisini kwake.

Amesema kuwa uzuiaji huo  ulifanyika  baada ya thathmini  ya ukusanyaji  wa mapato kwa kutumia  mashine za POS   kutoridhisha kwa kukusanya  mapato kiasi kidogo kulingana  na uwezo  mkubwa  wa kizuizi cha maliasili Kibiti.

Aidha amesema kuwa TAKUKURU ilisimamia  ukusanyaji  katika kituo hicho kuanzia Novemba 5 hadi 11 mwaka 2024 kwa masaa 24 nakukusanya Mil.12,089,760.

Kamanda Sadiki amesema baada ya kusimamia ukusanyaji wa fedha TAKUKURU imebaini kuwa baadhi ya  wakusanya ushuru kuletewa fedha  na wenye  mizigo ili wasitozwe malipo ya ushuru wa Serikali, baadhi ya wenye  magari yenye mizigo kuwasiliana  na  wakusanyaji ili wapite  bila kukaguliwa na wasilipe mizigo waliyoibeba,baadhi ya magari wakati wa ukaguzi walikuwa wanafungua buti na kuweka fedha  ya rushwa ili wakusanyaji wachukue  na wasiendelee na ukaguzi na Kisha  war Uhuru  magari hayo kupita.

"Wakusanyaji  wamepewa mwanya  mkubwa  wa kukadiria kiasi cha malipo cha kulipia katika mizigo inayopita,hivyo baadhi ya mizigo mikubwa imekuwa ikitozwa ushuru mdogo,baadhi ya  bidhaa ambazo haziruhusiwi kusafirishwa zimekuwa zikipitishwa usiku  na kutoa fedha ili wasichukuliwe hatua" amesema Kamanda Sadiki.

Wakati huohuo Kamanda Sadiki amesema kuwa katika kipindi tajwa TAKUKURU Pwani wamepokea jumla ya malalamiko 60 kati ya hayo  malalamiko 37 yalihusu rushwa  na taarifa hizo zimeshughulikiwa kwa  mujibu wa sheria kwa kuanzisha  uchunguzi ambao upo katika hatua mbalimbali za uchunguzi.

Taarifa 23 zilizobaki  ambazo hazikuhusu rushwa zineshughulikiwa kwa njia ya  uelimishaji,uzuiaji,ushauri na kuhamishiwa idaa nyingine. 

Taarifa zilizopokelewa ni TAMISEMI 11,michezo1,utalii1,Polisi4,ardhi
10,maji1, Mahakama 2,binafsi3,Elimu8,Viwanda5 Ujenzi4,Afya4,Siasa2, maendeleo  ya jamii 3 na ushirika1.

Aidha Kamanda  Sadiki amesema kuwa TAKUKURU  Pwani  katika kipindi hiki imefanikiwa  kufungua  jumla ya kesi mpya 24 Mahakamani  na kesi 13 washtakiwa wametiwa hatiani.

Akizungumza  kuhusu mikakati ya TAKUKURU kuanzia Januari  hadi Machi 2025 Kamanda Sadiki  amesema kuwa  wamejipanga  kuendelea  kutoa elimu kuhusu madhara ya rushwa katika uchaguzi mkuu kupitia semina, mikutano ya hadhara na vipindi vya redio ili kuwafikia wadau wote.

"Tutaendelea  kufanyan udhibiti wa mapato ya serikali na usimamizi wa rasilimali kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo  ,tutaendelea kupokea  taarifa za vitendo vya rushwa kufanya uchunguzi na kufikisha watuhumiwa Mahakamani" amesema  Kamanda Sadiki. 

Post a Comment

0 Comments