Mtindo huu wa vazi ambao huvaliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan umekuwa gumzo ndani na hata nje ya nchi huku watu wa rika zote, jinsia zote n wameanza kuiga mtindo huo unaofahamika kama “Samia Style.”
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti ametoa msisitizo kwamba Samia Style si kwa wanawake tu, hata wanaume wanaweza kuivaa kama alivyo vaa yeye
"Ni mwendo wa kujiamini, unadhifu na heshima katika mavazi.”amesema.
"Mtindo huu umevuka mipaka ya siasa na kuingia mitaani, ofisini, na hata kwenye mitoko ya kawaida" amesema.
""Watu wengi wanavutiwa na mavazi yenye heshima, rangi tulivu, na ushungi wa kipekee unaotajwa kuwa nembo ya Rais Samia" amesema DC Magoti.

0 Comments