SERIKALI YAZITAKA MAMLAKA ZINAZOSIMAMIA KITUO CHA MAFUNZO YA JESHI LA UHIFADHI MLELE KUFANYA MABORESHO YA CHANGAMOTO ZILIZOPO


Na Hamis Dambaya, Mlele Katavi

Serikali imeziagiza mamlaka na taasisi zinazosimamia na kutumia kituo cha mafunzo ya Jeshi la Uhifadhi kilichopo Mlele Mkoani Katavi kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo hicho.

Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) wakati akifunga mafunzo ya watumishi wa taasisi za uhifadhi zinazotoa mafunzo ya Jeshi la Uhifadhi wa wanyamapori na misitu yaliyofanyika kwa miezi mitatu   kwa lengo la kuwabadilisha watumishi waliojiunga na taasisi hizo hivi karibuni kutoka katika mfumo wa kiraia kwenda mfumo wa Kijeshi. 

Mhe. Kitandula amesisitiza kuwa ni muhimu taasisi hizo kuboresha miundombinu inayoklabili kituo hicho ikiwemo huduma za afya, barabara,maeneo ya kujifunzia,vifaa pamoja na kuhakikisha kituo hicho kinatumia nishati safi ya kupikia.

Mheshimiwa Kitandula amewapongeza wahitimu wote na kuwataka kutumia mafunzo hayo katika kuhakikisha kuwa wanalinda rasilimali za umma kwa uadilifu,uzalendo,uaminifu na kufuata sheria na taratibu zote za serikali.
Akizungumza kwa niaba ya Makamishna wa Uhifadhi zilizoko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamishna wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt.
 Elirehema Doriye amesema maelekezo yote yaliyotolewa na serikali yatafanyiwa kazi kwa kuunganisha nguvu ya taasisi zinazotumia kituo hizo ambazo ni  TANAPA,TFS,NCAA na TAWA.  
 Wahitimu wakisoma risala  walimweleza  Naibu Waziri uwepo wa changamoto hizo ambapo wamesema kwamba ikiwa maboresho hayo  yatafanyika   yataongeza tija na ufanisi wa kujifunza kwa wanafunzi na wakufunzi kutumia muda wao vizuri wa mafunzo.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo  hayo.
Mratibu wa mafunzo hayo kutoka wizara ya Maliasili na Utalii Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Fidelis Kapalata ameeleza kuwa jumla ya wanafunzi 231 wamehitimu mafunzo ya mabadiliko ya utendaji kutoka muundo wa kiraia na kwenda katika muundo wa kijeshi.

Post a Comment

0 Comments