Mlezi wa Twarika lkadiriya (Islam) wa Mkoa wa Pwani Alhaji Mussa Mansour ameahidi kuchimba visima viwili vya maji kwa wakazi wa Kata ya Pangani iliyopo Wilaya ya Kibaha Mjini.
Ahadi hiyo ya Alhaji Mansour imekuja baada ya kupokea maombi kutoka kwa uongozi wa Msikiti Kata ya Pangani ambayo inakabiliwa na ukosefu wa maji kwa muda mrefu sasa.
Alhaj Mansour ametoa ahadi hiyo leo tarehe 24 Januari 2025 katika Msikiti wa Kata ya Pangani mara baada ya ibada ya swala ya Ijumaa.
Aidha Alhaji Mansour amesema kuwa atatekeleza ahadi yake kwani anatambua umuhimu wa maji safi katika kufanya ibada kadhalika na mahitaji ya kila siku na kwenye jamii nzima kwa ujumla.
Alhaji Mansour ambaye pia mlezi wa Twarika lkadiriya Mkoa wa Pwani amewakumbusha waumini wa dini ya Kiislam kuwaombea Viongozi wakuu wa nchi yetu na Mungu awape afya njema ili waendelee kutuongoza vyema.
Alhaji Mansour akizungumza na waumini hawapo pichani mara baada ya sala ya ijumaa kwenye Msikiti wa Kata ya Pangani leo tarehe 24 Januari 2025.
0 Comments