Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo ametoa rai kwa Jeshi la Zimamoto kutoa elimu endelevu kwa wananchi kwamba wajenge nyumba zao kwa kuzingatia kujenga milango (mageti) yatakayo ruhusu kupitisha magari ya zimamoto na kuachana na tabia ya kujeng a mageti na kuweka urembo mwingi ambao pindi kunapotokea majanga inakua vigumu kupitika na kufanya uokozi.
"Nimeona watu wengi siku hizi wanajenga uzio kisha kwenye lango kuu la kuingia kwenye nyumba zao wanaweka urembo juu kishungi ambacho pindi kunapotokea majanga ya moto gari kubwa za uokozi zinashindwa kupita na kutoa msaada kwa wahusika natoa rai wananchi tujenge na kuremba nyumba zetu huku tukizingatia kuweka tahadhari ya kupitika pindi kunapotokea majanga ya moto" amesema Dkt.Jafo.
Mhe.Jafo amesema hayo leo Desemba 17 wakati alipotembelea banda la Jeshi la Zimamoto ambapo alikua mgeni rasmi kwenye maonesho ya nne ya Viwanda biashara na uwekezaji yanayoendelea kwenye viwanja vya Stendi ya zmani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.
Imeelezwa kuwa ni sharti kila nyumba kuwa na mlango na dirisha la dharura kwa sababu itasadia kurahisisha uokozi pindi kunapotokea majanga ya moto.
SSGT Joyce Kapinga wa Jeshi la Zimamoto Kibaha pichani juu amesema kuwa wananchi na wawekezaji wote wanapaswa kuchukua tahadhari za kujilinda na majanga ya moto ,amesema hayo wakati akitoa elimu kwa wananchi waliofika kwenye maonesho hayo .
" Nyumba kuwa na mlango na dirisha la dharura ni muhimu sana kwa uokozi kwa sababu endapo nyumba imejengwa bila ya kuwa na sehemu za dharura za kutokea na moto ukatokea milango hujibana na inakuwa ngumu kuwaokoa watu waliomo ndani hivyo Jeshi la Zimamoto tunatoa rai kwa wananchi wote nchini wazingatie hilo na unapojenga nyumba yako wewe mwenyewe ndiyo utakua unajua wapi kuna mlango wa dharura ama dirisha wananchi wazingatie hili ili kuweza kujiokoa na kuokolewa" amesema SSGT.Kapinga.
Wakati huohuo amesema kuwa wakati umefika kwa kila mwananchi kutoishi ndani na mitungi ya gesi kwa sababu ni hatari kubwa kwa sababu mtungi unaweza kuvuja gesi kusambaa na kuleta mripuko kwa sababu gesi ikisha sambaa ndani kitendo cha kuwasha taa au simu kinaweza kusababisha mripuko kwakua gesi inaripuka na kiwango kidogo cha joto.
"Ni muhimu kuweka mtungi wa gesi nje na ujengewe kibanda cha zege huku mpira wake ukitakiwa kuchimbiwa chini na kupitishwa kwenye bomba la chuma ambalo litakua nankazi ya kuzuia kuleta madhara na uripukaji na endapo mtungi utakuwa nje ni rahisi kunapotokea janga kuweza kuua njaa ya moto ndani kwa kuufunga na kuzuia gesi isiweze kusambaa"
amesema Kapinga.
Amesema katika kuepuka hilo kwa sababu wapo watu ambao tayari wameshajenga nyumba zao zikiwa hazina mifumo ya kujikinga na moto ameshauri kwa watu wote kufunga vifaa ambavyo vitang'amua endapo kuna viashiria vya moto kwa kutoa mlio na kusisitiza kwamba Jeshi la Zimamoto
haliuzi vifaa hivyo bali vinapatikana kwenye maduka ambayo wauzaji wake wamepata mafunzo kutoka kwao.
"Kuna vifaa vya kufunga na pia tunadhauri vifungwe sebuleni ambako ndiko kuna matumizi mengi ya vifaa vya umeme kamwe kifaa hicho kisifungwe jikoni "amesema Kapinga.
"Vifaa hivyo vya kung'amua kuna moto vinauzwa kwa mawakala na kwa upande wa bei amesema inategemea na kifaa hicho kinatoka nchi gani, pia kuna poda vyote vinapatikana kwa wauzaji ambao tumewapa.mafunzo na kuwakagua" amesema Kapinga.
Bendi ya JKT Ruvu wamenogesha maonesho hayo.
0 Comments