TANDAU AFUNGA MAFUNZO YA JUDO FILBERT BAYI

Wahitimu  wa mchezo wa Judo wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu wa TOC Meja Mstaafu wa JWTZ Filbert Bayi  ,Mgeni rasmi Makamu  wa Rais TOC Henry  Tandau.
Makamu wa Rais TOC  Henry Tandau akimkabidhi zawadi Kocha wa Judo nchini Uturuki Erdal  Dogan
Kamati  ya Olimpiki Tanzania (TOC) imeipongeza nchi ya Uturuki kwa kuwapatia Mkufunzi aliyetoa mafunzo kwa walimu wa mchezo wa Judo nchini.

 Makamu wa Rais  (TOC) Henry Tandau  amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya walimu wa mchezo huo yaliyofanyika kwenye shule ya Filbert Bayi.

Tandau amesema kuwa mafunzo hayo yameendeshwa na mkufunzi mwenye uwezo mkubwa na kuwapati mbinu nzuri walimu wa mchezo huo.
Kwa upande wake Katibu wa (TOC) Filbert Bayi amesema kuwa walimu hao wazingatie mafunzo hayo ili kuendeleza mchezo huo kupitia mashuleni.
Rais wa chama cha Judo nchini (JATA) Zaidi Omary amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa mchezo wa judo.
Akisoma risala ya washiriki wa mafunzo hayo Geophrey Mtawa amesema kuwa wanaiomba serikali kuwapatia magodoro na mafunzo ya mara kwa mara. 
Mafunzo hayo ya siku 10 yamesherikisha walimu 24 wa mchezo wa Judo kutoka Bara na Visiwani.
Mchezaji Asiatu Juma  
Judo ambaye ni miongoni wa wahitimu  wa mafunzo hayo amesema kuwa anaahidi kwenda kuwahamasisha mabinti ili waupende mchezo wa Judo pamoja na kusaka vipaji  katika Shule mbalimbali. 

Post a Comment

0 Comments