UTU RUN YAFANA VIWANJA VYA FARASI OYSTERBAY DAR

Wizara  ya Mambo ya Ndani ya  Nchi wameichangia  Taasisi ya Utu Kwanza Mil.2 ikiwa ni katika kuunga mkono jitihada za Taasisi hiyo  kutoa msaada wa Kisheria kwa wananchi walioko Mahabusu na Magerezani nchini.  
Akizungumza  kwenye hafla  ya maadhimisho ya miaka miwili ya Taasisi  ya Utu kwanza aliyekuwa mgeni rasmi
 Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uangalizi wa Wafungwa wa Kifungo Cha Nje kutoka Wizara ya Mambo Ya Ndani ya Nchi Charles Francis Nsanze  amemwakilisha Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni  na amemkabidhi mchango wa Mil.2 kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Utu Kwanza Shehzada Walli.

Akizungumzia kuhusu fedha  zilizotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani amesema ni kwa  ajili ya kuchangia dawati la  utoaji wa huduma za kisheria kwa wafungwa na mahabusu nchini ambao hawana uwezo.

Nsanze amesema kuwa jamii wanapaswa kuwa na ufahamu mkubwa kuwa ndugu zao walioko Magereza  ipo siku watarudi uraiani baada ya kumaliza vifungo  vyao hivyo waache tabia ya kuwatenga  kwani wengi ambao wamemaliza vifungo vyao pindi wanaporudi uraiani ndugu na jamaa zao huwatenga na kuwanyima haki ya kuishi kwa amani huku wakichangia kuwasababishia msongo wa mawazo. 
"Wafungwa wengi wanaporudiuraiani baada  ya kumaliza vifungo vyao wengi hukumbana nai yanyapaa,kukosa ajira jambo ambalo wengine hulazimika kufanya  matuko ya uhalifu na kurudi tena Gerezani wanakoona ndiyo sehemu sahihi kwao kuishi jamii wanapaswa kupewa elimu ya kuishi kwa upendo bila kuwatenga ndugu zao walio fungwa na kumaliza vifungo"amesema Nsanze.

"Jamii ,Mashirika  mbalimbali  ya kutetea  haki za binadamu  na Viongozi  wa dini wa made hebu yote wanao wajibu wa kutoa elimu ya kuacha unyanyapaa kwa ndugu zao ambao walikua wafungwa na kuishi vizuri pindi wanaporudi uraiani" amesema Nsanze
Msemaji wa Kampuni  ya Mafuta ya ameru Bi Sima Mittal ametoa pongezi kwa Uongozi wa Utu Kwanza kwa kuandaa  hafla hiyo.
Mbio hizo za 'Utu kwanza Run' zimefanyika kwa mara ya pili ikiwa ni  maalumu kwa ajili ya kuchangia  fedha za kusaidia  msaada wa dawati la  kisheria kwa watu wasiokuwa na uwezo waliopo  Magereza  na Mahabusu.

Hafla hiyo imepambwa  na  mbio za  baiskeli za  120Km huku    60Km. zilizoanzia Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani  hadi Viwanja vya Farasi vilivyopo Ostarbay Jijini Dar es salaam ambapo washiriki wengine wamekimbia  21Km. mbio za 10Km  na 5 Km
 Wakati huohuo  Walli  amesema kuwa wanahitaji kiasi cha
Mwenyekiti  wa Taasisi ya Utu Kwanza  ambaye pia ni Mratibu  wa 'Utu Kwanza Run'  Shahzada Walli amesema kuwa ndani ya mwaka mmoja tangu walipoanza  kutoa huduma hiyo kwa watu  ambao hawana uwezo wa kujitetea walioko Mahabusu na magerezani  wamefanikiwa kusaidia Watanzania 300 kwa kutoa huduma hiyo.

Aidha Wali amesema kuwa katika mafanikio hayo ndani yake kuna changamoto  zimejitokeza kwa sababu Mahakama imesitisha wao kwenda Magerezani  na Mahabusu kuzingumza na wahitaji ili waweze kuwapa msaada wa Kisheria.

Mwisho amewashukuru  wadhamini  ambao ni Meru,ASAS na wengineo
Mazoezi mepesi ya viungo yakiendelea katika Viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam Oktoba 6,2024
Wakufunzi wa Mazoezi  wakiwa jukwaani.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Utu Kwanza Shehzada Walli akiwa amesimama meza kuu mbele ya mgeni rasmi ambaye amemwakilisha Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani Hamad Masauni  ambaaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Huduma za Uangalizi wa Wafungwa wa Kifungo Cha Nje kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Francis Nsanze   kabla ya kumkabidhi zawadi maalumu kutoka Utu Kwanza kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam 06,Oktoba, 2024.
Baadhi ya wakimbiaji kutoka Kampuni ya Meru wakiwa kwenye mazoezi mepesi ya viungo katika Viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam. 

Wakimbiaji wa Km60 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Wa Idara ya Huduma za Uangalizi wa Wafungwa wa Kifungo Cha Nje kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Francis Nsanze.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Utu Kwanza Shehzada Walli akizungumza  na Waandishi wa Habari hawapo  pichana Oktoba 6,2024 katika Utu Run iliyoanzia na kumalizika Viwanja vya Farasi Oysterbay Jijini  Dare es Salaam
Mtangazaji wa Habari za Michezo Kituo Cha ITV na Radio One ambaye pia alikua mkimbiaji wa mbio za baiskeli Km120 Amri Massare akiteta jambo na Mwenyekiti wa Utu kwanza Shehzada Walli mara baada ya kuasili katika Viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Oktoba 6,2024.

Post a Comment

0 Comments