WATANZANIA ASILIMIA 80 KUFIKIWA NA ELIMU YA FEDHA

Afisa Sheria Mwandamizi Kurugenzi ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Ramadhani Myonga, akitoa elimu ya fedha kwa wananchi katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani.
Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha , Bw. Stanley Kibakaya, akitoa elimu ya fedha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia taasisi za fedha zilizosajiliwa wanapochukua mikopo ili kuwawezesha kuondokana na mikopo umiza pamoja na umuhimu wa kuzingatia mapato na matumizi ili wajiwekee akiba, wakati Maafisa wa Wizara ya Fedha walipokuwa wakitoa elimu ya fedha kwa wananchi katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani.
Wananchi wakichangia mada katika majadiliano baada ya mafunzo ya elimu ya fedha kutolewa na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha, walipowasili kwa ajili ya programu ya elimu ya ya fedha kwa wananchi, katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Kibaha -Pwani)
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na Maafisa kutoka Wizara ya Fedha waliowasili kutoa elimu ya fedha kwa wananchi, kuhusu usimamizi wa fedha binafsi, dhamana za mikopo, riba pamoja na uwekezaji, katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani.
Afisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Uwekezaji wa UTT AMIS, Bw. Rahim Mwanga, akiwaelekeza wananchi kuhusu mifuko ya uwekezaji inayopatikana katika Mfuko wa Uwekezaji wa UTT Amis na jinsi wanavyoweza kunufaika na fursa za uwekezaji, wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha iliyotolewa na Maafisa kutoka
Wizara ya Fedha, katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani.

Post a Comment

0 Comments