wakiwa na Makocha ambao ni Maafisa na Askari wa Majeshi nchini Uwanja wa Mpira wa miguu Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Makocha wa timu za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakiwa katika mazoezi ya namna walivyofundishwa na Wataalamu watatu kutoka nchini Uholanzi.Leo 10 Septemba ,2024 katika Uwanja wa Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Mafunzo yaliendelea katika Uwanja wa Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Makocha wa timu za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakiwa katika mazoezi ya namna walivyofundishwa na Wataalamu watatu kutoka nchini Uholanzi.Leo 10 Septemba ,2024 katika Uwanja wa Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Mafunzo yaliendelea katika Uwanja wa Mbweni Jijini Dar es Salaam.
MKUU wa Majeshi nchini Jenerali Jacob Mkunda (CDF) kupitia uratibu wa Baraza la Michezo la Majeshi ya Ulinzi Dunia Conseil International du Sports Military imewaleta wakufunzi na wataalamu kutoa mafunzo kwa makocha nchini ikiwa na lengo la kuwaaendeleza Maafisa wa Jeshi na Askari wenye taaluma ya michezo.
"Mafunzo haya yataimarisha mahusiano mazuri kati ya Tanzania na nchi ya Uholanzi (Netherlands)".
"Dhamira ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania ni kupata waalimu wazuri watakao saidia timu za JWTZ zinazoshiriki katika ligi mbalimbali nchini na kimataifa.
Hayo yamesemwa leo 11,Septemba,
2024 na Kocha Rajab Bwamkuu kutika JWTZ alipozungumza na Waandishi wa Habari kwenye Uwanja wa JKT Mbweni uliopo Jijini Dar es Salaam.
Kocha Rajab Bwamkuu amezungumza kwa niaba ya wenzake amesema wanatoa shukran kwa Mkuu wa Majeshi CDF Jacob Mkunda kwa kuona umuhimu wa kuwaleta wakufunzi hao ambapo mbali na wakufunzi hao kutoka nje pia Shirikisho la Soka nchini (TFF) wamekuwa wakitoa mafunzo mbalimbali.
"Waalimu hawa wakigeni wapo mbali kimafunzo na wanavifaa vya kisasa hivyo tanatoa ahadi ya kufanya vizuri katika kuhakikisha timu za Majeshi na Taifa zinafanya vizuri" amesema Kocha Bwamkuu.
Aidha Bwamkuu ametaja majina ya Wakufunzi hao kutoka nchini Uholanzi (Netherlands) ni Rob Van Belkom,
Hans Feensta na Sigi Careera.
"Mafunzo haya ni ya wiki mbili na ijumaa jioni yatafungwa rasmi hii inatokana na mahusiano mazuri ya Chama Cha Mpira wa miguu Cha majeshi" amesema Bwamkuu .
Makocha ambao ni Maafisa na Askari wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Wakufunzi hao.
0 Comments