MNADHIMU MKUU WA JWTZ LUTENI JENERALI SALUM HAJI OTHUMAN AMEISHUKURU KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othuman ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi na Mambo ya Nje ya Kisiwa cha Ushelisheli kwa kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na JWTZ katika harakati za ukombozi barani Afrika.

Luteni Jenerali Othuman ameyasema hayo alipotembelewa na kamati hiyo Makao Makuu ya JWTZ Msalato jijiji Dodoma tarehe 03 Septemba 2024.

Naye  Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Francois Adelaide amesema JWTZ limekuwa msaada mkubwa sana kwa nchi nyingi za kusini kwa Afrika.

Amesema nchi yake itaendelea kukuza diplomasia ya Ulinzi hasa kwenye mafunzo, mazoezi pamoja na kubadilishana ujuzi katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kukabiliana na majanga.
Mnadhimu Mkuu wa  Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othuman akiwa  katika  picha ya  pamoja  na Kamati  ya Kudumu ya Mambo ya Nje ya Kisiwa Cha Ushelisheli walipotembelea  Makao Makuu ya JWTZ Msalato Dodoma. 


Post a Comment

0 Comments