SERIKALI, SEKTA BINAFSI WAZINDUA MADAWATI YA URATIBU WA NGOs

Na WMJJWM, Dodoma

Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi imezindua madawati ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Sekta hiyo.

Akizindua madawati hayo Septemba 04, 2024 kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Jinsia Felister Mdemu amesema, ushirikiano huo utafanikisha malengo ya kuwa na taifa lenye maendeleo endelevu na wananchi wenye ustawi thabiti. 

Felister amesema, Madawati hayo yatakuwa ni kiungo kati ya Sekta Binafsi, Serikali na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kuwa mwanzo wa kufungua fursa mpya, kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wa miaka mitano  2021/2022-2025/2026


Post a Comment

0 Comments