RAIS MHE. DKT. SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA CHINA MHE. XI JINPING



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping pamoja na Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakishuhudia uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya kuboresha reli ya TAZARA katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing, tarehe 4 Septemba, 2024.
(PIHA ZOTE NA IKULU)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake wakiwa kwenye kikao cha pamoja na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping na ujumbe wake katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing, tarehe 4 Septemba, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan l amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping katika ukumbi wa The Great Hall of the People O4 Septemba  , 2024.

Katika mazungumzo yao, Rais Dkt. Samia amesema uhusiano wa nchi hizo mbili ni muhimu na ametoa wito wa kuendelea kudumisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali pamoja na kuendeleza ushirikiano katika Mpango wa Kuendeleza Miundombinu na Kukuza Uwekezaji (Belt and Road Initiative) ili kuleta manufaa yanayoonekana kwa wananchi.

Rais Dkt. Samia ametoa wito kwa sekta binafsi nchini China kuwekeza Tanzania katika uzalishaji wa vyanzo vya nishati mbadala na miundombinu ya usambazaji.

Katika mkutano huo, Rais Xi alisema kuwa China iko tayari kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati yake na Tanzania ili kuleta manufaa zaidi kwa nchi zote mbili na kuendeleza uhusiano wa kihistoria ulioasisiwa na waasisi na kurithiwa na vizazi vya sasa.

Rais Xi pia amesema China inaiona Tanzania kuwa ni mfano mzuri wa mahusiano kati ya nchi zinazoendelea katika muktadha wa ushirikiano wa China na nchi za Afrika.

China na Tanzania zimekubaliana kuendelea kubadilishana uzoefu na kupeana mafunzo katika maeneo mbalimbali ya kiserikali. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping katika ukumbi wa The Great Hall of the People kabla ya kuanza mazungumzo jijini Beijing, tarehe 4 Septemba, 2024.

Post a Comment

0 Comments