Mhe. Sangu amesema kwa mujibu wa sera ya ajira toleo la pili la mwaka 2008 inaelekeza kuwa ajira zote zipatikane kwa ushindani .
‘’Maombi yamekuwa mengi sana kati ya nafasi 12,000 zilizotangazwa za kada ya afya zaidi ya vijana 47,000 wameomba huku kwenye walimu jumla ya vijana waliomba ni 200,000 kati nafasi za ajira za ualimu 11,015 zilizotangazwa hivyo hakuna njia nyingine ya kupata watumishi pasipo kushindanisha’’ amesema.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu kutoka kwenye Taasisi mbalimbali za Serikali ambao wamechaguliwa kuwa wanajopo wa kuendesha zoezi la usaili wa mahojiano ya ana kwa ana kwa wasailiwa kada ya afya unaendelea katika mikoa mbalimbali nchini.Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza na wataalamu kutoka kwenye Taasisi mbalimbali za Serikali ambao wamechaguliwa kuwa wanajopo wa kuendesha zoezi la usaili wa mahojiano ya ana kwa ana kwa wasailiwa kada ya afya unaendelea katika mikoa mbalimbali nchini.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Dkt. Cairo Mwaitete mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kuzungumza na kushuhudia wataalamu kutoka kwenye Taasisi mbalimbali za Serikali ambao wamechaguliwa kuwa wanajopo wa kuendesha zoezi la usaili wa mahojiano ya ana kwa ana kwa wasailiwa kada ya afya Jijini Arusha.
0 Comments