Katibu wa Chama Cha Wafugaji Tanzania Daniel Matayo akizungumza na Waandishi wa Habari waliofika kwenye hafla hiyo .
Kiongozi wa Kimila wa Maasai Mkoa wa Pwani Laigwanani Faed Ngayoki Kasokwa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Wilaya ya Bagamoyo Wilson Ole Dongo almaarufu kama Mjeshi akizungumza jambi.
Mnec Hamoud Abuu Jumaa akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kupokea barua ya kuwa Mlezi wa Chama Cha Wafugaji Kanda ya Mashariki ambayo ni Dar es Salaa, Tanga Morogoro na Pwani.
Na Mwandishi Wetu, Ruvu Darajani
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kupitia Wazazi Hamoud Abuu Juma leo Septemba 2,2024 ametangazwa kuwa mlezi wa Chama Cha Wafugaji Tanzania kwenye tukio lililofanyika Viwanja vya Ruvu Darajani Kibaha Vijijini ,Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
Akizungumza mara baada ya kupokea rasmi barua hiyo Mnec Hamoud ambaye pia ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kibaha Vijijini msimu uliopita amesema kuwa kuwa tukio hilo kubwa ni la kihistoria na ameipokea kwa furaha kubwa ombi la kuwa mlezi wa Wafugaji katika Kanda ya Mashariki knayounganisha Mikoa ya Tanga, Morogoro,Dar es Salaam na Pwani .
"Nimepokea barua ya uteuzi kwa shangwe kubwa kwakuwa mimi ni mtu ninayependa kuacha alama nawaahidi kuwa tutaondoa taswira mbaya ya kwamba wafugaji ni wakorofi,nitahakikisha wanakua wafugaji wa kisasa kwa muda mfupi na kubwa zaidi ni kumaliza kabisa migogoro kati ya wakulima na wafugaji ili wote waweze kuishi kwa amani kama jinsi alivyo agiza Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kwaulimbiu isemayo wakulima na wafugaji watunzwe" amesema Mnec Jumaa.
Mnec Jumaa amesema kuwa anashukuru Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumaliza tatizo la wafugaji wa Ngorongoro kwa hekima ya hali ya juu naahidi kwamba tutafanya kazi usiku na mchana kumaliza tofauti baina ya wafugaji na wakulima.
Akielezea kuhusu uchaguzi ujao wa serikali za mitaa amesema kuwa anawahamasisha wakulima na wafugaji wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la mpigakura ikiwa no pamoja na kuchukua fomu ili waweze kuchukua nafasi kwa sababu serikali inahitaji kupata wenyeviti wazuri ambao watakua wasaidizi wazuri kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Katibu wa Chama Cha Wafugaji Tanzania Daniel Matayo amsema huko nyuma kulikua na migogoro mingi baina ya wakulima na wafugaji ikiwa ni pamoja na maeneo ya malisho kuvamiwa na wakati mwingine wafugaji kulisha katika mashamba ya wakulima, hivyo basi kwa kuona changamoto hiyo ndipo Chama tukawiwa kumteua mlezi wa kwanza katika Kanda ya Mashariki ambaye atasaidiana na Mlezi wa Taifa Joseph Makongoro wote kwa pamoja tunaungana na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kaulimbiu isemayo tutunzane aliyoitoa Mvomero Mkoani Morogoro.
Katibu amesisitiza kwa kusema kuwa katika kumaliza migogoro kwa wakulima.na wafugaji watasimamia kupima maeneo ya malisho ya wafugaji na kuchimba maji sababu malisho ni biashara na endapo itatokea mfugaji amelisha katika eneo la mkulima achukuliwe hatua kwa jina lake na siyo kuwachafua wengine.
Katibu Matayo amesema kuwa katika miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan wafugaji wamepata zaidi ya lita Bil.52 huku majosho 756 yamejengwa katika Halmashauri zote nchini pamoja na kupimiwa wafugaji kupimiwa ardhi hivi sasa wafugaji wanaishi kwenye nyumba za umeme mifugo hailiwi na fisi kama zamani.
Naye Kiongozi wa Kimila wa Maasai Mkoa wa Pwani Laigwanani Faed Ngayoki Kasokwa amesema kuwa suala la Wafugaji kumpata mlezi ni baraka kubwa kwa Chama Cha Wafugaji na kwa sasa wanaishi vizuri wakulima na wafugaji na endapo kunatokea changamoto huwa wananzimaliza katika ngazi za viongozi na wameacha kupelekana Polisi kwa kuwa wamekua wakizitatua kwa umoja na Ushirikiano.
Wakati huohuo Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Wilaya ya Bagamoyo Wilson Ole
Dongo almaarufu kama Mjeshi amesema ni heshima kubwa kwa Wafugaji kupata mlezi wao hivyo wana imani kubwa na mnec Hamoud wafugaji na wakulima wana imani kubwa na yeye .
Baadhi ya Laigwanani wakiwa kwenye sherehe hiyo ya kumpokea mlezi wa Wafugaji katika Kanda ya Mashariki Mnec Abuu Jumaa Humoud hafla iliyofanyika Ruvu Darajani,Kibaha Vijijini Mkoani Pwani. Baadhi ya Wafugaji wakiingia kwa msafara kwenye viwanja vya Ruvu Darajani Septemba 2 ,2024.
Mnec Abuu Jumaa Hamoud katikati anayefuata ni Katibu wa Chama Cha Wafugaji Tanzania David Matayo na Mwenyekiti wa Wafugaji Bagamoyo Wilson Ole Dongo(Mjeshi).
Jamii ya wafugaji wakiwa kwenye shamrashamra za mapokezi ya mlezi wao Mnec Abuu Jumaa Hamoud zilizofanyika Ruvu Darajani, Septemba 2,2024.
0 Comments