KILELE MAADHIMISHO MIAKA 60 YA JWTZ YAACHA GUMZO

Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan  akiwa kwenye gari maalumu la kijeshi  akiwapungia mkono Maafisa na Askari  kweye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kushoto   ni Mkuu wa Majeshi   CDF Jacob Mkunda . 
(PICHA ZOTE NA IKULU)
Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),katika kilele kilichofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Septemba 1,2024 Jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Wananchi  waTanzania wakiwa kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)Septemba  1,2024 katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. 
Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kilele kilichofanyika  Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  Septemba 1,2024.
Kutoka kushoto ni Amiri Jeshi Mkuu Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa na  Mkuu wa Majeshi CDF Jacob Mkunda kwenye maadhimisho  ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Usalama la Wananchi Tanzania (JWTZ)alipokagua gwaride Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, Septemba 1 ,2024.
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  akikagua gwaride la Maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Septemba 1,2024.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  akiwa na viongozi  mbalimbali  kwenye maadhimisho   ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyofanyika  Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.Septemba 1,2024.
Katika maadhimisho  hayo baadhi ya  zana  za Kijeshi zimeoneshwa.



Amiri Jeshi Mkuu mbalimbali  wakati wa kilele cha Maadhimisho ya kutimiza miaka 60 kwa Jeshi hilo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Septemba, 2024. Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan akizindua kitabu cha Miaka 60 ya JWTZ  katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.Septemba 1,2024.
Amiri Jeshi Mkuu Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan  akimkabidhi Mkuu wa Majeshi  Generali Jacob Mkunda Kitabu  cha  miaka 69 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)mara baada ya kukizindua Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam Septemba 1,2024.

Akizungumza  katika maadhimisho  hayo CDF Mkunda amemshkuru Mwenyeezi Mungu  kwa kuwapa kibali cha kutuwewaka  hapa,pia amemshukuru Mhe.Rais kwa kukubali  mualiko wa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kileke cha miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  na kufanikisha siku hii kwa niaba ya Maafisa , Askari  na watumishi  wa umma wote tunatoa shukrani zetu za dhati kwako"amesema CDF Mkunda. 

Aidha CDF  Jacob  Mkunda amesema kuwa  zana zote  za  Kijeshi  zilizoonesha na zisisizooneshwa zote zimenunuliwa katika  katika awamu zote  za uongozi zilizopita kwa chombo hiki muhimu sana cha Ulinzi wa nchi na kamwe hatuwezi kuwasahau  hata kidogo kwa mchango wao  kwetu Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lililoasisiwa Septemba 1,1964 amesema a  CDF Mkunda .

"Sisi Wanajeshi  hupata  hamasa  kubwa hasa  pale tunapoona  raia wazalendo wakituunga mkono kwani wao ndiyo chachu  ya sisi kuwa na ari ya kukabiliana na  changamoto  mbalimbali kwa sababu tunawapenda na tunawathamini  tuaahidi kuwa tutaendelea  kujitoa kwa ajili yao" amesema CDF  Mkunda  .

Wakati huohuo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania  Jacob Mkunda  amewapongeza Maafisa  na Askari wote wa JWTZ waliolitumikia  Jeshi hilo  kwa weledi  katika kipindi chote cha miongo sita.

Amesema kuwa JWTZ wanaahidi kulinda  uhuru , Katiba  na mipaka ya nchi pamoja na kudumisha uzalendo.

Post a Comment

0 Comments