Baadhi ya Wabunge wakiwa katika kikao cha Baraza hilo.
Na Mwandishi Wetu ,Chalinze
HALMASHAURI ya Chalinze Mkoani Pwani imetenga kiasi cha Bil.17 ambazo zimetengwa kwa ajili ya msimu wa fedha kipindi cha 2024-25.
Akizungumza katika kikao cha Madiwani Chalinze robo ya nne ya mwaka kilichofanyika leo Septemba 6 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Mwenyekiti Hassan Mwinyikondo amesema kuwa "Tumejipanga kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo Kujenga Kituo Cha mafuta 'Petrol Station' kwa ajili ya kuongeza vyanzo vya mapato ndani ya Halmashauri hiyo.
Mwinyikondo amesema kuwa pia wamepanga kujenga vyoo kituo cha mabasi cha Chalinze ikiwa ni katika kuboresha utoaji huduma kwa abiria.
Taarifa hiyo imetolewa baada katika kikao cha Baraza la Madiwani Cha Kota ya nne ambacho kimemalizika kwamafanikio ya asilimia 100.
Mwinyikondo amesewataka wataalamu wote kushirikiana na Madiwani katika kutekeleza miradi iliyopo sanjari na kuikamilisha kabla ya uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.
"Madiwani na Wataalamu tunakwenda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo ni wajibu wenu kushuka chini kwa wananchi mkatatue kero zao"amesema Mwinyikondo.
Kuhusu ukarabati wa Kituo Cha Afya Lugoba ambacho kilianza 1972,kutokana na uchavu wake tunatarajia kukifanyia ukarabati tumeomba gari na tunatarajia utaanza Septemba mwaka huu,"Tumeomba gari hivyo tunatarajia kukifanyia ukarabati ili kukiboresha" amesema.
Aidha ameziomba Taasisi mbalimbali kutoa taarifa zaomapema
kwa baraza la madiwani ili waweze kupitia kwa wakati.
Meneja TANESCO Chalinze Salima Muharam amesema kuwa watapigania ndani ya mwakani shule hiyo inapatiwa umeme.
"Tayari mkandarasi ameshapatiwa mikataba na tayari imepelekwa kwa Mwanasheria Mkuu baada ya hapo kazi itaanza haraka.
0 Comments