“WAZIRI UMMY AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA KLABU YA AFRICAN SPORTS” AITAKA IPAMBANE KUCHEZA LIGI DARAJA LA KWANZA MSIMU UJAO




 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu katikati akimkabidhi vifaa vya michezo ambavyo ni viatu Mwenyekiti wa timu ya African Sports  Awadhi Salehe Pamba ikiwa ni kuipa motisha timu hiyo kufanya vizuri kwenye michuano wanayoshiriki ili waweze kufanya vizuri na hatimaye kuweza kurejea daraja la kwanza na Ligi kuu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Meja Hamisi Mkoba
                   WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu   kushoto akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports Awadhi Salehe Pamba leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo
    WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu   kushoto akiteta jambo na  Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports Awadhi Salehe Pamba leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kushoto ni  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Meja Hamisi Mkoba
 Halfa ya makabidhiano ikiendelea
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu   kushoto akimkabidhi viatu hivyo Nahodha wa timu ya African Sports Mohamed Kidiwa
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu ametoa vifaa vya michezo kwa timu ya African Sports ya Tanga yenye thamani ya zaidi ya milioni 1.5 ikiwa ni mkakati kabambe wa kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki na hatimaye kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Makabidhiano hayo yalifanyika leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga wakati wa ufunguzi wa timu ya wanawake ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya wilaya ya Tanga ambapo alisema vifaa hivyo vitakuwa ni chachu ya timu hiyo kuweza kufikia malengo yao.
Aliyasema hayo mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa timu hiyo katika halfa iliyoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa klabu ya African Sports ambapo alisema dhamira yake kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inarejea ligi daraja la kwanza na ile ya Coastal Union ihakikisha msimu ujao inarudi Ligi kuu.
“Niseme tu sisi tumejipanga kuhakikisha tunazirejesha timu hizi kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara tukianzia na timu ya Coastal Union lakini ndugu zangu African Sports mhakikishe mnarudi ligi daraja la kqwanza na baadae ligi kuu “Alisema
Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo,Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports,Awadhi Salehe Pamba alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia msaada huo ambao utakuwa ni chachu kwao kuweza kufikia malengo yao kutokana na changamoto hiyo kwisha.
Alisema msaada uliotolewa na Waziri utakuwa chachu kubwa kwao kuweza kufikia malengo yao waliojiwekea ya kuhakikisha wanarudi ligi kuu kwani ndio ndoto yao kubwa ambayo wamekuwa wakiiwaza kila wakati.
“Mh Waziri tukushukuru sana katika hili umetupa nguvu ya kuweza kupambana na tuna kuhaidia kuhakikisha tunairudisha timu Ligi daraja la kwanza na hatimaye ligi kuu.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Post a Comment

0 Comments