Bw,Patrick Fata ambaye ni Mhelimishaji kutoka BOT akielekeza na kutoa elimu namna ambavyo unaweza kutambua Noti bandia. |
Meza kuu ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Chato Shaaban Ntarembe. |
Maafisa wa BOT wakifuatilia maelezo ya Meneja Msaidizi wa Idara ya Uhusiano wa BOT, Vicky Msina wakati alipokuwa akielezea juu ya elimu ambayo wanaitoa kwa viziwi. |
Bw,Patrick Fata ambaye ni Mhelimishaji kutoka BOT,akisisitiza swala la alama za fedha ambazo zinakuwepo kwenye noti. |
Kifaa ambacho kinatumika kuangalizia noti bandia na ile ambayo ni ya harari. |
Noti ambazo zinakuwa zimeharibiwa zikiwa kwenye mafungu fungu lenye rangi nyekundi ni elfu kumi na yenye rangi ya blue ni elfu tano. |
Benki kuu ya
Tanzania (BOT)imekutana na kundi
la watu wenye ulemavu wa kutokusikia na
wale ambao hawaoni Wilayani Chato lengo
likiwa ni kuwapatia na elimu ya utambuzi wa Noti bandia Wilayani humo.
Akizungumza
kwenye semina ambayo imefanyika kwenye ukumbi wa KKKT Wilayani Humo,Meneja
msaidizi wa idara ya uhusiano wa BOT, Vicky Msina alisema elimu wanayoitoa
imelenga kuwawezesha viziwi kutambua alama za usalama zilizopo katika noti ili
kuzitofautisha na noti bandia wanapokuwa katika shughuli zao kwani mtu yeyote
akikutwa na noti bandia ni kosa la jinai, hivyo wanawapa mafunzo ili wasikumbwe
na kadhia hiyo.
“Ni muda sasa walituomba kuwapa
mafunzo na hii ni kutokana na wengi wao kutokujua noti bandia wamekuwa
wakijikuta wanabambikiwa na pia wanapo kwenda benki kupeleka fedha zao wahudumu
huwadharau na wakati mwingine kwa wale wanao kwenda kuchukua fedha hupatiwa noti
chafu jambo ambalo lilitusukuma kuwaelimisha juu ya hatua za kufuata ilikupatiwa
haki zao za msingi kwenye huduma hizo,”alisema Msima.
Mwenyekiti wa Kituo cha Sanaa na
Utamaduni kwa Viziwi Tanzania (Kisuvita), Habibu Mrope alisema kuna tatizo kubwa la kutotambua noti bandia
kwa Walemavu hali ambayo imechangia kuwarudisha nyuma kwani wanapokutwa na noti
hizo huchukuliwa hatua za kisheria.
Hata
hivyo kutokana na tatizo hilo Mkuu wa wilaya ya Chato Shaaban Ntarambe aliwaahidi
watu ambao wanamatatizo ya kutokusikia
kufunguliwa kwa shule ambayo itawasaidia kujifunza lugha za alama kwania ya
kuboresha mawasiliano kwenye jamii.
“Idadi ya wilaya yetu kuna Viziwi
347 ambapo ni sawa na asilimia 90 ya watu wenye ulemavu wa kusikia hawajui
lugha za nyakati upekee idadi hii ni kubwa
sana ni lazima Serikali ifanye jitihada za kuwa kwamua watu hawa ambapo kwa kushirikisha
wadau mbali mbali, nitahakikisha ujenzi wa shule hiyo unaanza mara moja,”alisisitiza
Tarambe
Kwa
upande wake mmoja wa washirki wa semina hiyo, Issa Pastori, mkazi wa Buziku wilayani
humo alishukuru kupatiwa mafunzo hayo na kwa upande wa suala la uanzishwaji wa shule
maalum ya lugha za alama ameomba mchakato huo uanze haraka kwani ni mkombozi kwao.
0 Comments