BODI YA WADHAMINI YA TANAPA IKIONGOZWA NA MWENYEKITI WAKE JENERALI (MSTAAFU) WAITARA YATEMBELEA HIFADHI YA KATAVI


Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), na wajumbe wa bodi hiyo, wakikaribishwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Katavi, Mhifadhi Izumbe Msindai, walipowasili kwenye hifadhi hiyo leo Septemba 28, 2017.

BODI ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa bodi, Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara, leo Septemba 28, 2017 imetembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa ajili ya kukagua utendaji kazi ambapo ilipata fursa ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Hifadhi Izumbe Msindai.

Bodi imepongeza utendaji kazi katika Hifadhi ya Katavi hususani suala zima la kupambana na ujangili na juhudi zinazofanywa katika kuongeza idadi ya watalii hifadhini.Aidha, Jenerali Waitara aliutaka uongozi wa hifadhi kuongeza jitihada katika kukabiliana na changamoto za mifugo ambayo ni kubwa kwa Katavi na pia alipongeza uongozi wa mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali mstaafu Raphael Muhuga kwa ushirikiano mkubwa anaotoa kwa hifadhi katika kupambana na mifugo hifadhini.

Mapema kabla, bodi iliweza kutembelea kituo cha mafunzo cha Mlele na kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Kituo Mhifadhi Genes Shayo na kupata nafasi ya kuongea na askari wapya wanaoendelea na mafunzo katika kituo hicho.

Jenerali Waitara aliwataka askari hao kuwa na nidhamu, uwajibikaji, bidii na uzalendo katika mafunzo yao na kuwa ni lazima waonyeshe kuiva ili waweze kupambana vilivyo na changamoto ya ujangili katika Hifadhi za Taifa nchini.
Jenerali Waitara, akionyesha kitu wakati yeye na wajumbe wa bodi walipotembelea enelo wanakohifadhiwa Viboko

Jenerali Waitara akizungumza na askari wanaopatiwa mafunzo kwenye kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi


Baadhi ya wajumbe wa bodi waliofiatana na Jenerali Waitara

Baadhi ya askari wanaopatiwa mafunzo ya ulinzi wa wanayamapori kwenye kituo cha mafunzo cha Mlele wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi za Taifa, (TANAPA), Jenerali mstaafu George Marwa Waitara (hayupo pichani), alipowatembelea leo Septemba 28, 2017
Baadhi ya askari wanaopatiwa mafunzo ya ulinzi wa wanayamapori kwenye kituo cha mafunzo cha Mlele wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi za Taifa, (TANAPA), Jenerali mstaafu George Marwa Waitara (hayupo pichani), alipowatembelea leo Septemba 28, 2017
Jenerali Mstaafu George Waitara, (kushoto) akipkewa na viongozi wa Hifadhi ya Taifa Katavi, alipowasili mapema leo.
Geofrey Adroph BLOGGER P.O.BOX 24793, Mob: +255 755 274953 /+255 713 363965, Email: pamojapure@gmail.com. Blog: http://www.pamoja.co.tz/ DAR ES SALAAM, TANZANIA

Post a Comment

0 Comments