|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Peter Serukamba (kulia) pamoja na Wajumbe wengine mara baada ya kuwasili katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) kwa ajili ya kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017. |
|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii, Mhe. Peter Serukamba pamoja na Wajumbe wengine mara baada ya
kuwasili katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) kwa
ajili ya kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017. |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA), Dkt. Helbert Makoye akiwaeleza jambo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii, mara baada ya
kuwasili katika taasisi hiyo kwa
ajili ya kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017. |
|
Mkuu wa Kitengo cha Muziki wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) Bi.Rhoda Mitanda (kushoto) akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Kudumua ya Bunge ya Huduma na Maendeleo kuhusu namna vifaa mbalimbali vya muziki na kazi zake mara walipowasili katika Taasisi hiyo kwa
ajili ya kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017. |
|
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii, wakionyeshwa vifaa vitumikavyokatika uhariri wa kazi za sanaa walipoingia katika moja ya Studio ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) kujionea utendaji kazi wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017. |
|
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii, Mhe. Peter Serukamba akiongea na Wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) mara baada ya
kuwasili katika Taasisi hiyo kwa
ajili ya kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017. |
|
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii pamoja na Wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakijadiliana wakati wa kikao 17 Machi, 2017. |
|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiongea na Wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakati wa kikao cha kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017. |
|
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii wakitoa maoni yao wakati wa kikao cha kujadili na kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017. |
|
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii pamoja na Wafanyakazi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakisikiliza maoni mbalimbali yaliyolenga kuiboresha taasisi hiyo wakati wa kikao cha kujadili na kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017. |
|
Wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakionyesha umahiri wao katika sanaa mbalimbali mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii baada ya kumalizika kikao kilicholenga kukagua mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017. |
|
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi pamoja na Wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) mara baada ya kumalizika kwa ziara iliyolenga kufanya ukaguzi wa mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo, 17 Machi, 2017. |
(Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM)
0 Comments