WAKAZI WA PONGWE WATOA SHUKRAN KWA JWTZ

Wakazi wa kijiji cha Pongwe Msungura kilichoko Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani wamelishukuru Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa msaada mkubwa iliyoutoa kwa watoto wao.
Akizungumza kwa niaba ya  wazazi  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Pongwe Msungura Bw Joel Kajonga amesema JWTZ limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi na wanafunzi wa kijijini hapo.
 Kamanda wa Kikosi cha 8 kinachokwenda kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Luteni Kanali Theofili Nguruwe amesema JWTZ ni jeshi la wananchi hivyo litaendelea kutoa msaada kila itakapowezekana.
Mbali na msaada huo pia wataalam wa afya wa JWZT waliweza kutoa matibabu na elimu ya afya kwa wazazi wa kijiji hicho.
Msaada uliotolewa shuleni hapo ni mahindi kwa ajili ya chakula, maharagwe, sukari, madaftari, kalamu, viatu, mabegi vyote vikilenga kuongeza morari wa kusoma kwa wanafunzi.

Post a Comment

0 Comments