BASATA YAPIGA MARUFUKU WIMBO WA NEYWAMITEGO

Baraza  la Sanaa la Taifa  (BASATA) leo limepiga marufuku wimbo  mpa wa msanii Ney wa Mitego kutokana na kutokuwa na maadili yanayopaswa .
Akizungumza na vyombo vya habari leo Katibu Mkuu Mtendaji BASATA Geofrey Mngereza amekiri kuwa wimbo huo umetungwa kinyume na maadili ya Mtanzani, huku akipiga marufuku kutopigwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchin.
Wimbo huo ambao umeachiwa sikuchache  na msanii huyo umeonekana kutokuwa na maudhui mazuri kwa jamii nchini.

"Kazi ya msanii ni kuelimisha  na kuburudisha sasa huu hauna lolote na haufai"alisisitiza Mngereza. 

Wakati huohuo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi hilo.

Waziri Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo huo, na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.

Akiongea na Wandishi wa Habari muda huu mjini Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO, na kumshauri Msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile Wakwepa  Kodi, Wauza Unga, Wabwia Unga, Wezi pamoja na watu wengine wasio na maadili mema katika jamii. 

Post a Comment

0 Comments