Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Simai Mohammed Said akizungumza na waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vya Tanzania na Nje wakati wa kutowa kwa taarifa kwa kukamilika kwa matayarisho ya Tamasha hilo linaloaza leo katika viwanja vya ngome kongwe mji mkongwe wa Zanzibar kwa kutowa burudani ya muziki wa kiasili wa Afrika na kuwashirikisha Wasanii zaidi ya 400 kutoka sehemu mbalimbali ya Afrika na kutowa shukrani kwa Wadhamini waliojitokeza kutowa udhamini wao kwa hali na Mali wakiwemo Kampuni ya Simu ya Zantel, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip Malindi Zanzibar.
Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar DJ Yussuf Mahmoud, akizungumza wakati wa mkutano huo wa waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip Malindi Zanzibar na kuwataja washiriki watakaopamba Tamasha Wasanii kutoka sehemu mbalimbali wamethibitisha kushiriki na tayari wako Zanzibar kwa ajili ya Tamasha hilo litakaloazia kwa maandamano maalumu yatakayowashirikisha washanii hao yataazia katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani na kupita katika mitaa mbalimbali ya mji wa Unguja hadi kumalizikia katika viwanja vya Mambo Club Ngome Kongwe Zanzibar.
Mkuu wa Kampuni ya Zanztel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha akizungumza wakati wa mkutano huo wa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kutoka nje ya Zanzibar wanaoshiriki kuripoti habari za Tamasha hilo linaloaza leo katika viwanja vya ngome kongwe Zanzibar kwa maonesho mbalimbali ya Wasanii kutoka Nchi za Afrika likiwa n a Kau Mbiu #Africa United.
Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo na Waandishi wa Habari akiwawakilisha Wadhamini wa Tamadha hilo.
Waandishi wakifuatilia mkutano huo wa kuanza kwa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar.
Msanii kutoka Nchini Seychelles Grace Barbe akiwa katika ukumbi wa mkutano huo na waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli Golden Tulip Malindi Zanzibar.
Waandishi wakifuatilia mkutano huo.
0 Comments